Pata taarifa kuu

Uswisi yatangaza msaada wa zaidi ya euro milioni 600 kwa Ukraine, rekodi ya msaada wa kijeshi

Uswisi imetangaza, siku ya Jumanne Februari 20, rekodi mpya ya msaada wa kijeshi kwa Ukraine katika mfumo wa vifaa vya kiasi cha taji (fedha za Uswisi) bilioni 7.1, sawa na takriban euro milioni 633, wakati Kiev inajitahidi kukabiliana na Moscow.

Hivi katibuni Ukraine iliishutumu Urusi kwa kuwanyonga wafungwa wawili wa vita wa Ukraine. (Picha ya kielelezo)
Hivi katibuni Ukraine iliishutumu Urusi kwa kuwanyonga wafungwa wawili wa vita wa Ukraine. (Picha ya kielelezo) REUTERS - ALINA SMUTKO
Matangazo ya kibiashara

 

"Sababu ya kuendelea kuunga mkono Ukraine ni suala la ubinadamu na adabu. Urusi imeanzisha vita haramu, visivyochochewa na visivyoweza kutetewa,” Waziri wa Ulinzi Pål Jonson ametangaza katika mkutano na waandishi wa habari.

Jeshi la Ukraine kwa sasa liko katika hali "ngumu kabisa" kuwakabili wanajeshi wa Urusi ambao wako kwenye mashambulizi mashariki na kusini mwa Ukraine baada ya kuuteka mji wa Avdiivka wikendi hii, Kiev ilikiri kupotea mji huo siku ya Jumatatu.

"Hali ni ngumu sana katika sehemu kadhaa katika uwanja wa vita, ambapo askari wa Urusi wamejizatiti vilivyo katika vita hivi. Wanajaeshi wa Urusi wanapata nafasi ya kusonga mbele katika vita hivi kufuatia kucheleweshwa kwa msaada wa nchi za Magharibi kwa Ukraine, Rais Volodymyr Zelensky alitangaza siku ya Jumatatu, Februari 19, katika ujumbe wake wa kila siku. Aliongeza kuwa nchi yake haina silaha za kivita na inahitaji  vifaa vya kivita vya ulinzi wa angani kama vile silaha za masafa marefu.

Mkuu wa nchi wa Ukraine pia alibaini kwamba kuzuiwa kwa mpaka na Poland na wasafirishaji wa malori na wakulima wa Poland kunaonyesha "kuzorota kwa mshikamano" kwa nchi yake.

Katika uwanja wa vita, askari wa Urusi, ambao wamepata ushindi wao wa kwanza tangu kutekwa kwa Bakhmut mnamo mwezi Mei 2023 kwa kuchukua udhibiti wa Avdiïvka, katika mkoa wa mashariki wa Donetsk, walifanya shambulio mashariki na kusini, limeelezea jeshi la Ukraine.

Katika sehemu ya kusini ya uwanja wa vita, "adui amefanya majaribio kumi bila kufanikiwa dhidi ya ngome za vikosi vya ulinzi vya (Ukraine) katika eneo (la kijiji) cha Robotyne. Hapa, hali inabadilika, adui anatoa moto mkali,” amesema Dmytro Lykhovy, msemaji wa jeshi la Ukraine katika eneo hili.

Mashambulizi ya Urusi katika sehemu hii ya vita ya kusini yalianza wikendi hii wakati jeshi la Urusi lilipoteka Avdiïvka, takriban kilomita 150 kaskazini mashariki mwa Robotyne, baada ya miezi minne ya mashambulio ya mara kwa mara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.