Pata taarifa kuu

Italia: Mazishi ya Victor Emmanuel wa Savoy kufanyika Turin

Mazishi ya Victor Emmanuel wa Savoy , mtoto wa mfalme wa mwisho wa Italia, aliyefariki siku ya Jumamosi, yatafanyika Jumamosi Februari 10 katika kanisa la Superga, karibu na Turin (kaskazini mwa Italia), imeripoti televisheni ya kidini Tv2000.

Victor Emmanuel wa Savoy, mwanamfalme wa Italia, huko Milan, Septemba 28, 2006.
Victor Emmanuel wa Savoy, mwanamfalme wa Italia, huko Milan, Septemba 28, 2006. AP - GIUSEPPE ARESU
Matangazo ya kibiashara

 

"Mazishi ya Victor Emmanuel yatafanyika Jumamosi saa 9:00 alaasiri saa za Italia, atakapozikwa kwenye kilima cha Turin", televisheni ambayo ni mali ya Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI) imeandika kwenye mtandao wa X.

Kanisa la Superga lilijengwa mwanzoni mwa karne ya 18 kwa agiza la Duke Victor Amédée II wa Savoy, kumshukuru Bikira Maria kwa kulishinda jeshi la Ufaransa la Louis XIV huko Turin mnamo 1706 wakati wa Vita vya mamlaka vya Uhispania.

Sehemu kubwa ya familia ya Savoy wamezikwa katika kanisa hili.

Hafla ya mazishi ilifanyika katika siku zilizotangulia huko Reggia di Vednaria Reale, jumba la kifalme la Venaria, pia karibu na Turin, moja ya makazi ya familia ya Savoy, iliyoorodheshwa kama Urithi wa Dunia wa UNESCO tangu mwaka 1997, kulingana na vyombo vya habari.

Victor Emmanuel wa Savoy alifariki siku ya Jumamosi huko Geneva baada ya kukaa uhamishoni kwa muda mrefu.

Victor Emmanuel wa Savoy ambaye alizaliwa Februari 12, 1937 huko Naples, alikuwa mkuu wa Nyumba ya Savoy ambaye alishikilia kiti cha enzi cha Italia kutoka mwaka 1861 hadi mwaka 1946 na mtoto wa mfalme wa mwisho, Umberto II, ambaye alikuwa na cheo hiki tu kuanzia mwezi Mei hadi Juni 1946.

Aliondoka Italia akiwa na umri wa miaka 9, akiwa amefukuzwa pamoja na wazao wote wa kiume wa nyumba ya kifalme na Katiba ya 1946 kwa kuchukulia vikwazo dhidi ya ushirikiano wa babu yake, Victor Emmanuel III, pamoja na utawala wa kifashisti na kutia saini sheria za ubaguzi wa rangi.

Aliweza tu kurejea nchini Italia mnamo mwezi wa Desemba 2002, baada ya kuondolewa kwa hatua ya kukaa uhamishoni iliopigiwa kura na Bunge la Italia. Ili kupata afueni hiyo, ilimbidi aape kuwa mwaminifu kwa Jamhuri, ishara ambayo alikataa kwa muda mrefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.