Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Italia yashtumiwa kwa kuwatendea vibaya wahamiaji wa Sudan

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR) imeishtumu Italia siku ya Alhamisi kwa mazingira ya kukamatwa na kusafirishwa kwa raia wa Sudan ambao waliachwa wakiwa uchi miongoni mwa wahamiaji wengine. ECHR imetoa uamuzi katika kesi mbili zilizoletwa na Wasudan tisa waliowasili kwa njia ya bahari majira ya joto ya mwaka 2016.

Mahakama hiyo yenye makao yake mjini Strasbourg pia imepata ukiukaji wa Kifungu cha 3 kuhusiana na mmoja wa Wasudan ambaye alidai kupigwa wakati wa jaribio lingine la kuondolewa, na ikabainisha kuwa hakuna uchunguzi wowote ambao ulikuwa umefanywa.
Mahakama hiyo yenye makao yake mjini Strasbourg pia imepata ukiukaji wa Kifungu cha 3 kuhusiana na mmoja wa Wasudan ambaye alidai kupigwa wakati wa jaribio lingine la kuondolewa, na ikabainisha kuwa hakuna uchunguzi wowote ambao ulikuwa umefanywa. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kuhusu malalamiko ya walalamikaji wanne katika kesi ya kwanza, Mahakama imeamua kwa kauli moja kwamba kumekuwa na ukiukwaji wa Kifungu cha 3 cha Mkataba wa Ulaya wa Haki za Kibinadamu (kutendewa kinyama au kudhalilishwa). Mahakama inaona kwamba mazingira ya kukamatwa kwao na kusafirishwa kwao kwa basi yaliwasababishia watu hao dhiki na fedheha. Mahakama imeagiza Italia kuwalipa jumla ya euro 27,000 kwa uharibifu wa maadili, na euro 4,000 kwa gharama na matumizi.

Wahamiaji hao walilazimika kuvua nguo ili waweze kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu baada ya kukamatwa, lakini ECHR imeamua kwamba sababu hiyo haikuwa ya kutosha kuhalalisha kuwaacha uchi miongoni mwa wahamiaji wengine wengi, bila faragha yoyote na chini ya uangalizi wa polisi.

Pia walivumilia uhamisho wa muda mrefu kwa basi wakati wa joto sana lililoripotiwa mwaka huo, bila maji ya kutosha na chakula na bila kujua walikokuwa wakienda na kwa nini. Mahakama inasisitiza kwamba walibaki chini ya udhibiti wa polisi mara kwa mara, katika mazingira ya vurugu na vitisho, ambavyo lazima vilikuwa chanzo cha dhiki kwao.

Mahakama hiyo yenye makao yake mjini Strasbourg pia imepata ukiukaji wa Kifungu cha 3 kuhusiana na mmoja wa Wasudan ambaye alidai kupigwa wakati wa jaribio lingine la kuondolewa, na ikabainisha kuwa hakuna uchunguzi wowote ambao ulikuwa umefanywa.

Katika maamuzi yaliyotolewa siku ya Alhamisi, Mahakama, hata hivyo, imetoa uamuzi kwa kauli moja kwamba maombi manane kati ya tisa yasikubaliwe ambapo walalamikaji waliikosoa mamlaka ya Italia kwa kutozingatia hatari ya kuteswa kikatili ambayo wangejikuta wakikabiliwa nayo ikiwa wangerudishwa nchini Sudan. Walalamikaji wanne katika kesi ya kwanza hawana hatari tena ya kufukuzwa nchini na wanne kati ya watano katika kesi ya pili hawajathibitisha malalamishi yao vya kutosha, kwa mujibu wa Mahakama.

Kwa upande wa mlalamikaji ambaye ombi lake linaonekana kuwa limekubalika, Mahakama imehitimisha kwamba hakukuwa na ukiukwaji wa Mkataba wa Ulaya wa Haki za Kibinadamu kwa sababu mlalamikaji hakuonyesha kuwa yeye ni wa kabila linaloteswa na serikali ya Sudan baada ya kuwasilisha maombi yake kwa ECHR.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.