Pata taarifa kuu

Makubaliano yafikiwa kufungua mazungumzo ya Ukraine na Moldova kujiunga na EU

Wakati kukitarajiwa mkutano mrefu na mgumu wa kilele wa Ulaya juu ya upanuzi wa EU kwa Ukraine na Moldova, nchi 27 wanachama wa umoja huo umeamua siku ya Alhamisi, Desemba 14, baada ya saa chache tu, kufungua mazungumzo ya Ukraine na Moldova kujiunga na umoja huo. Uamuzi huo ulikaribishwa mara moja na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky. Huu ni mwanzo wa mchakato ambao utaendelea kuwa mrefu na ambao uliaminika kutishiwa na ukaidi wa Waziri Mkuu wa Hungary.

Baadhi ya viongozi wa Umoja wa Ulaya, Desemba 14, 2023 mjini Brussels, katika siku ya kwanza ya mkutano wao wa kilele.
Baadhi ya viongozi wa Umoja wa Ulaya, Desemba 14, 2023 mjini Brussels, katika siku ya kwanza ya mkutano wao wa kilele. REUTERS - YVES HERMAN
Matangazo ya kibiashara

Ni kupitia mitandao ya kijamii ambapo taarifa hiyo ilitangazwa Desemba 14, anaeleza mwandishi wetu maalum mjini Brussels, Daniel Vallot. Kwenye mtandao wa X (zamani ukiitwa Twitter), Charles Michel, Rais wa Baraza la Ulaya, ametangaza ufunguzi wa mazungumzo ya kujiunga na Ukraine na Moldova. “Ishara ya wazi ya tumaini kwa watu wao na kwa bara letu,” ameandika kiongozi huyo wa Ulaya.

Tangazo la makubaliano haya linakuja kwa mshangao. Tulitarajia hapa, Brussels, majadiliano marefu sana. Wengine hata walitaja uwezekano wa kulazimika kupanua mazungumzo haya hadi Jumamosi Desemba 16, au hata Jumapili Desemba 17.

Hungary yajizuia na yaghadhabishwa, Ukraine yaridhika

Mtazamo wa Hungary na makubaliano yanayoweza kufanywa na Viktor Orban, Waziri Mkuu, yalijumuisha pointi kubwa ya swali. Mkuu wa serikali ya Hungary alisema, mwanzoni mwa mkutano huu, kwamba anapinga ufunguzi wa mazungumzo haya ya kujiunga, akisema kuwa Ukraine haikuwa tayari na kwamba Ulaya itayumba.

Hatimaye, Viktor alijizuia kupiga kura. "Hungary haitaki kushiriki jukumu" kwa uchaguzi huu "usio na maana" wa nchi zingine 26 na "kwa hivyo imejizuia," alisema kwenye video iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Mwishowe, Viktor Orbán alichagua kutopiga kura ya turufu na kutumia kile tunachokiita hapa kujizuia kwa njia yenye kujenga, anaripoti mwandishi wetu wa Brussels, Pierre Benazet. Waziri Mkuu wa Hungary aliondoka kwenye chumba hicho wakati wengine 26 walipoamua kufungua mazungumzo ya kujiunga na Ukraine. Anaendelea kuelezea uamuzi huu kama usio na mantiki hasa kwa vile, kwake, Ukraine haijakidhi vigezo vitatu kati ya saba vya awali, ambavyo ni haki za walio wachache, vita dhidi ya rushwa na ushawishi wa viongozi madarakani.

Bado kutakuwa na hatua ya pili, pengine mwezi Machi, wakati mfumo wa mazungumzo utawekwa katika mkutano wa serikali kati ya nchi 27 wanachama. Hii inaacha tarehe mpya ya mwisho inayokaribia ya kutathmini kufuata kwa vigezo vyote vya awali.

Kwa hali yoyote, ni mafanikio kwa Umoja wa Ulaya, ambao ulitaka kutuma ishara kali ya uungwaji wake mkono wa kisiasa kwa Ukraine, ishara iliyokusudiwa kwa Ukraine yenyewe, lakini pia kwa Vladimir Putin. Na ishara hii inaimarishwa na uamuzi wa kufungua mazungumzo ya kujiunga na Moldova na kutoa hadhi ya nchi ya mgombea kwa Georgia.

Sasa inabakia kwa Wazungu kujaribu kukubaliana na Hungary juu ya msaada wa kifedha kwa Ukraine kuweka bahasha ya Euro bilioni 50 kwa miaka minne.

"Ushindi kwa Ukraine" na "Ulaya yote", anasema Zelensky

Volodymyr Zelensky anakaribisha habari hii kwa kuridhika na utulivu mkubwa. Kwenye mtandao wa X, rais wa Ukraine alichapisha ujumbe: "Ninamshukuru kila mtu aliyefanya kazi kufanikisha hili na kila mtu aliyesaidia. Ninawapongeza Waukraine wote siku hii. Pia naipongeza Moldova na binafsi (Rais) Maia Sandu. Historia imeandikwa na wale ambao hawachoki kupigania uhuru. "

Ukraine ilihitaji ushindi huu kwa upande wa kidiplomasia, kwani inatatizika kupata ufadhili ulioahidiwa na Marekani na inahofia kupasuka kwa uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa Urusi. Tangazo la makubaliano haya, kwa mtazamo huu, bila shaka ni habari njema sana kwa Kyiv.

Habari njema pia kwa Moldova, ambayo itanufaika na huduma sawa, na kwa Georgia, ambayo inapata hadhi ya mgombea kama inavyopendekezwa na Tume.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.