Pata taarifa kuu

Marekani kuihami Ukraine na vifaru vya M1 Abrams

Waziri wa usalama wa Marekani Lloyd Austin, amesema Ukraine inakaribia kuaanza kupokea vifaru vya kivita aina ya M1 Abrams kutoka kwa Washington, mpango unaokuja wakati huu Kyiv ikidaiwa kuaanza kusonga mbele katika uwanja wa mapambano.

US military personnel and M1 Abrams tanks in German ahead of war games in February 2020
US military personnel and M1 Abrams tanks in German ahead of war games in February 2020 AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Wawakilishi wa mataifa yanayoiunga mkono nchi ya Ukraine wanakutana nchini Ujerumani kujadiliana kuhusu mpango wa kutoa msaada mpya kwa Kyiv kuelekea hotuba ya rais Volodymyr Zelensky katika mkutano wa baraza kuu la Umoja wa mataifa.

Washington ilikuwa imeahidi kutoa vifaru 31 kwa Kyiv mwanzo mwa mwaka huu ikiwa ni sehemu ya msaada wa Dolla bilioni 43 wa kiusalama ulioahidiwa na Marekani tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwezi Februari mwaka wa 2022.

Waziri wa ulinzi wa Marekani amethibitisha hatua hiyo wakati kwa kikao cha nchi washirika wa Ukraine nchini Ujerumani
Waziri wa ulinzi wa Marekani amethibitisha hatua hiyo wakati kwa kikao cha nchi washirika wa Ukraine nchini Ujerumani AP - Michael Probst

Afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Marekani amesema sehemu ya kwanza ya vifaru hivyo itatumwa nchini Ukraine katika siku zijazo kabla ya mpango huo kumalizika katika kipindi cha wiki kadhaa.

Zelensky aliwasili Marekani siku ya Jumatatu, akiwatembelea wanajeshi wa Ukraine waliojeruhiwa hospitalini kabla ya hotuba yake ya Umoja wa Mataifa, ambayo ataitoa wakati wanajeshi wa nchi hiyo wakisonga mbele kwa mashambulio ya mwendo wa polepole na ya hali ya juu kuchukua maeneo yanayokaliwa na  Urusi kimabavu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.