Pata taarifa kuu

Nafaka: Kyiv anawasilisha malalamiko katika WTO dhidi ya Poland, Slovakia na Hungary

Ukraine imetangaza Jumatatu hii, Septemba 18, kwamba imewasilisha malalamiko kwa Shirika la Biashara Duniani dhidi ya nchi tatu za Umoja wa Ulaya, ambazo zimeongeza muda wa vikwazo vyao kuhusu kuagiza nafaka za Ukraine, licha ya kuondolewa kwa vikwazo vilivyoamuliwa na Brussels.

Tangu mwanzoni mwa mwezi bei ya nafaka imepanda kwenye soko la hisa la Paris, zaidi ya euro 175 kwa tani.
Tangu mwanzoni mwa mwezi bei ya nafaka imepanda kwenye soko la hisa la Paris, zaidi ya euro 175 kwa tani. ©Balint Porneczi/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Kiev imetangaza siku ya Jumatatu kwamba imewasilisha malalamiko kwa WTO dhidi ya nchi tatu za Umoja wa Ulaya - Poland, Slovakia na Hungary - ambazo zilingeza muda wa vikwazo vyao kuhusiana na kuagiza nafaka kutoka Ukraine, licha ya kuondolewa kwa vikwazo vilivyoamuliwa na Brussels.

"Ni muhimu kwetu kutambua kwamba nchi wanachama haziwezi kupiga marufuku uingizaji wa bidhaa za Ukraine," amebaini Waziri wa Uchumi Yulia Svyrydenko katika taarifa. "Hii ndiyo sababu tunawasilisha malalamiko dhidi yao," ameongeza.

Nafaka kwa bei nafuu

Mwishoni mwa mwezi Aprili, Tume ya Ulaya iliruhusu nchi tano wanachama (Poland, Hungary, Slovakia, Bulgaria, Romania) kuzuia uuzaji wa nafaka kutoka Kiukreni, mahindi, rapa na alizeti kutoka Ukraine ili kulinda wakulima wao. Kufuatia kuondolewa kwa ushuru wa forodha wa EU mnamo Mei 2022, nchi hizi ziliona kuongezeka kwa nafaka kwa bei iliyopunguzwa kutoka Ukraine, kushindwa kwa biashara barani Afrika au Mashariki ya Kati kwa sababu ya uvamizi wa Urusi.

Siku ya Ijumaa, Brussels ilisitisha marufuku hii ya muda, ikibaini hasa kwamba "upotoshaji wa soko" uliosababishwa na wingi wa nafaka za Ukraine "umetoweka". Kukaidi uamuzi wa Tume, yenye uwezo wa kufafanua sera ya kibiashara ya nchi Ishirini na Saba za Umoja wa Ulaya, Poland, Hungaria na Slovakia mara moja zilitangaza kwamba watadumisha marufuku yao kwa upande mmoja.

"Tunatumai kuwa nchi hizi zitaondoa vikwazo vyao na kwamba hatutahitaji kwenda mahakamani kwa muda mrefu kutatua mzozo wetu," waziri wa Ukraine alisisitiza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari. Romania "ilijutia" uamuzi wa Brussels lakini ilijiepusha na hatua zozote za upande mmoja huku Bulgaria ikikubali kuondoa vikwazo kwa jina la "mshikamano na Ukraine".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.