Pata taarifa kuu

Italia: Karibu wahamiaji 7,000 watua Lampedusa ndani ya saa 48

Meya wa kisiwa kidogo cha Italia cha Lampedusa, Filippo Mannino, amesema siku ya Alhamisi kwamba "katika saa 48 zilizopita, karibu wahamiaji 7,000" wamewasili kwenye kisiwa hicho. Meya ameiambia redio ya Italia RTL 102.5 kwamba "hatua ya kutorejea" imefikiwa na kwamba "kisiwa kiko katika mgogoro mkubwa."

Wahamiaji wakikusanyika nje ya kituo cha uendeshaji kinachoitwa "Hotspot" kwenye kisiwa cha Italia cha Lampedusa mnamo 14 Septemba 2023.
Wahamiaji wakikusanyika nje ya kituo cha uendeshaji kinachoitwa "Hotspot" kwenye kisiwa cha Italia cha Lampedusa mnamo 14 Septemba 2023. AFP - ALESSANDRO SERRANO
Matangazo ya kibiashara

Lampedusa haiwezi tena kustahimili wimbi la wahamiaji wanaowasili kwenye ufuo wake. "Katika saa 48 zilizopita, karibu watu 7,000 wameingia Lampedusa, ambayo imekuwa ikiwakaribisha kwa mikono miwili," ametangaza Alhamisi, Septemba 14, meya, Filippo Mannino, kwenye redio ya Italia RTL 102.5. "Hata hivyo, tumefikia hatua ya kutorejea na kisiwa kiko katika mgogoro mkubwa," amelaumu. "Ulaya na taifa la Italia lazima ziingilie kati mara moja kwa kuanzisha msaada wa haraka na operesheni ya kuwahamisha watu hawa."

Lampedusa, kisiwa kikubwa zaidi cha Italia, ambacho kinapatikana katika Bahari ya Mediterania, kati ya Tunisia, Malta na Sicily, kisiwa,  ni bandari ya kwanza ya inayowapokea wahamiaji wengi wanaotaka kuingia katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Kwa kawaida kisiwa hicho kina wakazi zaidi ya 6,000 tu.

Changamoto kwa serikali ya Giorgia Meloni

Picha zilizopigwa mapema wiki hii zilionyesha mistari ya boti zikingoja kutia nanga kwenye bandari ya Lampedusa.

Kituo cha wageni cha kisiwa hicho kina uwezo wa kupokea watu wapatao 400.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.