Pata taarifa kuu

Moto mkubwa zaidi kuwahi 'kurekodiwa katika EU' wakumba kaskazini mwa Ugiriki

Kwa zaidi ya siku kumi, eneo la Alexandroupoli, kaskazini mwa Ugiriki, limekuwa likikabiliwa na moto, ambao tayari umeharibu zaidi ya hekta 80,000 za mimea. Zaidi ya maafisa 400 kikosi cha Zima moto kwa sasa wametumwa kwenye eneo la tukio. Kuhusu moto huu, msemaji wa Tume ya Ulaya ametaja "moto mkubwa zaidi kuwahi kurekodiwa katika Umoja wa Ulaya". 

Moto mkubwa umeteketeza makumi ya maelfu ya hekta katika eneo la Evros kaskazini mwa Ugiriki hapa ilikuwa tarehe 29 Agosti 2023.
Moto mkubwa umeteketeza makumi ya maelfu ya hekta katika eneo la Evros kaskazini mwa Ugiriki hapa ilikuwa tarehe 29 Agosti 2023. REUTERS - ALEXANDROS AVRAMIDIS
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Athens, Joël Bronner

Moto huo bado haujadhibitiwa, kaskazini mwa Ugiriki, katika eneo la Evros, karibu na mpaka wa nchi kavu na Uturuki, ulianza Agosti 19. Kulingana na Copernicus, mpango wa anga wa Umoja wa Ulaya, moto huo umeharibu eneo la miti mikubwa kuliko ukubwa wa Jiji la New York.

Kwa upande wake, serikali ya Ugiriki ilitangaza mfululizo wa hatua siku ya Jumanne, ikiwa ni pamoja na kazi ya fidia na udhibiti wa mafuriko ambayo moto mbalimbali msimu huu wa joto unaweza kufadhiliwa.

Ukichochewa na upepo na joto, moto huu ambao ulianza karibu na jiji la Alexandroupoli - na ambao maafisa wa kikosi cha Zima moto wameuhusisha na radi - kisha kuenea haraka katika eneo la Evros, hasa katika msitu wa Dadia, mbuga ya kitaifa inayojulikana kwa kuhifadhi wanayama wengi wa aina yake hususan ndege wengi wa kuwinda, ikiwa ni pamoja na tai, na ambayo ni ya mtandao wa Ulaya wa Natura 2000.

Baada ya mkutano wa serikali ya Ugiriki siku ya Jumanne, Waziri wa Mazingira, Theodoros Skylakakis, alihakikisha kwamba maeneo makubwa yaliyoteketea kwa moto karibu na mji wa Athens na Alexandroupoli yanapaswa kufikiiwa upywa kwa upandaji miti.

“Kama ilivyokuwa kwa mioto ya awali, sasa tunazindua katika maeneo yaliyoathiriwa taratibu za kudhibiti mmomonyoko wa ardhi na hatari ya mafuriko. Yaani tutaweka mabwawa na kufanya kazi za ufundi za aina nyingine ndio kipaumbele. "

Kwa zaidi ya maafisa 400 wa kikosi cha Ziama Moto ambao bado wanafanya kazi katika eneo la Evros, kipaumbele kinasalia kuzima moto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.