Pata taarifa kuu

Visa vya moto: Operesheni kubwa zaidi ya uokoaji yafanywa kwenye kisiwa cha Rhodes

Ugiriki inakabiliwa na wimbi jipya la joto wikendi hii, na viwango vya juu vinavyoweza kufikia hadi 45ºC. Tangu mwanzoni mwa juma, halijoto ya juu pia imependelea kuchochea mikasa ya moto kote nchini. Kwa wakati huu, hali mbaya inaripotiwa katika kisiwa cha Rhodes, karibu na pwani ya nchi jirani ya Uturuki.

Mawingu ya moshi kutoka kwa moto wa nyikani ukipanda kuelekea angani kwenye kisiwa cha Rhodes, Ugiriki, Jumamosi, Julai 22, 2023.
Mawingu ya moshi kutoka kwa moto wa nyikani ukipanda kuelekea angani kwenye kisiwa cha Rhodes, Ugiriki, Jumamosi, Julai 22, 2023. AP - uncredited
Matangazo ya kibiashara

Nchini Ugiriki, wazima moto wamerekodi mikasa mipya 46 ya moto ndani ya masaa 24. Moto huo umetanda Jumapili hii kwa siku ya sita mfululizo nchini humo. Katika kisiwa cha Rhodes, wakati wa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, moto ulifika kijiji cha Laerma, ukiteketeza nyumba na kanisa, kulingana na kituo cha ERT TV na shirika la habari la Ugiriki ANA. Hoteli nyingi pia zimeathirika na moto huo ukisambaa hadi katika vijiji vya pwani vya Kiotari na Gennadi. Waokoaji wameendesha "operesheni kubwa zaidi ya uokoaji kuwahi kufanywa nchini Ugiriki" kwenye kisiwa hiki cha kitalii katika visiwa vya Dodecanese, msemaji wa polisi ameliambia shirika la habari la AFP.

Siku ya Jumamosi, watu waliahamishwa katika angalau maeneo manne, wakati wazima moto zaidi ya 200 walikuwa wakipambana na moto kwenye maeneo ya tukio, anaripoti mwandishi wetu huko Athens, Joël Bronner. Ujumbe wa uhamishaji ulipokelewa, kwa mfano, saa sita mchana na wakazi wa vijiji vya Lardos na Pylonas, si mbali na mji mdogo wa kitalii wa Lindos, maarufu kwa eneo lake la kiakiolojia.

Mapambano ya kudhibiti moto huo yatachukua siku kadhaa zaidi, kulingana na mamlaka. 

Watu 30,000 wameondoka katika maeneo yanayotishiwa na moto

Baadhi ya uokoaji pia ulifanyika kwa njia ya bahari, hasa kwa msaada wa boti tatu za walinzi wa pwani. Kulingana na mamlaka ya eneo hilo, watu wapatao 30,000 waliweza kuondoka katika maeneo yanayotishiwa.

Viwango vya joto vinavyozidi 44°C vinatarajiwa Jumapili nchini Ugiriki. Kulingana na uchunguzi wa kitaifa wa hali ya hewa, nchi hii "huenda" inapitia wimbi refu zaidi la joto katika historia yake. "Tuna uwezekano wa kupata wimbi la joto la siku kumi na sita hadi kumi na saba, ambalo halijawahi kutokea katika nchi yetu," Kostas Lagouvardos, mkurugenzi wa utafiti ameiambia ERT. "Tunahitaji umakini kabisa (...) kwa sababu nyakati ngumu hazijapita," Waziri Mkuu Kyriakos Mitsotakis alionya sikyu ya Ijumaa.

Miaka miwili iliyopita, wakati wa wimbi lingine la joto, moto ulikuwa haudhibitiki katika kisiwa cha Ugiriki cha Euboea. Zaidi ya hekta 50,000 za msitu ziliteketea kwa motoi.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.