Pata taarifa kuu

Raia wawili wa Urusi wanazuiliwa nchini Poland

Nairobi – Poland inasema inawazuilia raia wawili wa Urusi kwa madai ya kusambaza stakabadhi za propaganda za kundi la Wagner" katika mji wa Warsaw na Krakow, miji mikubwa miwili nchini Poland, waziri wa mambo ya ndani imeeleza.

Poland imeimarisha ulinzi kwenye mpaka wake na Belarus
Poland imeimarisha ulinzi kwenye mpaka wake na Belarus via REUTERS - 12 BRYGADA ZMECHANIZOWANA
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarfia ya Poland kwenye ukurasa wa X, watu hao wawili wameshtakiwa kwa makosa ya ujasusi na kwa sasa wanazuiliwa bila ya kutoa maelezo zaidi kuhusu watu hao wanaozuiliwa.

Poland hivi majuzi imeonya juu ya uwezekano wa uchochezi kutoka kwa kikundi cha mamluki kilichoko katika nchi jirani ya Belarus, na ilisema kwamba kwa kujibu itaongeza viwango vya askari wake kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili hadi 10,000.

Vyombo vya habari vya Poland wiki iliyopita viliripoti kuhusu kuonekana kwa vibandiko vilivyo na nembo ya Wagner na maandishi kwa Kiingereza yanayosoma "Tuko hapa, jiunge nasi", pamoja na misimbo ya QR inayoelekeza kwenye tovuti ya Kirusi ya kikundi cha mamluki.

Kulingana na gazeti la kila siku la Gazeta Wyborcza, vibandiko hivyo viliripotiwa kwa polisi na wakazi wa Krakow na Warsaw.

Wizara ya mambo ya ndani haikubainisha iwapo watu hao walikamatwa kuhusiana na usambazaji wa stika hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.