Pata taarifa kuu

Urusi imesitisha mkataba wa usafirishaji wa nafaka katika bahari nyeusi

Nairobi – Urusi imesema imesitisha mkataba wa usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine kwenda katika nchi za Afrika, Mashariki ya Kati na Asia ambako tishio la njaa linaloongezeka na bei ya juu ya vyakula imewafanya watu wengi zaidi kuwa maskini.

Urusi inasema itarejelea mpango huo wakati matakwa yake yatakapotekelezwa
Urusi inasema itarejelea mpango huo wakati matakwa yake yatakapotekelezwa © REUTERS - MEHMET CALISKAN
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov ametangaza kusitisha mpango huo katika wito wa mkutano na waandishi wa habari, akiongeza kuwa Urusi itarejea kwenye makubaliano hayo baada ya matakwa yake kutekelezwa.

"Wakati sehemu ya makubaliano ya Bahari Nyeusi kuhusiana na Urusi itatekelezwa, Urusi itarejea mara moja kwenye utekelezaji wa mpango huo," Peskov alisema.

Makubaliano hayo yalioongozwa na umoja wa mataifa na Uturuki yaliwezesha usafirishaji wa chakula kutoka katika Bahari Nyeusi baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

sehemu kubwa ya mataifa ya Afrika yamekuwa yakinufaika kutokana na mpango huo
sehemu kubwa ya mataifa ya Afrika yamekuwa yakinufaika kutokana na mpango huo © Emrah Gurel /AP

Urusi imelalamika kuwa vikwazo vya usafiri wa meli na bima vimetatiza usafirishaji wake nje ya nchi.

Ujerumani imetoa wito kwa Urusi kurejea katika mkataba wa nafaka wa Bahari Nyeusi ambao Moscow ilisema "ulimalizika" saa chache kabla haujakamilika, ikibaini kuwa ni muhimu kwa usalama wa chakula.

"Tunaendelea kutoa wito kwa Urusi kuruhusu kurefushwa zaidi kwa mkataba wa nafaka," msemaji wa serikali Christiane Hoffmann aliwaambia waandishi wa habari, akiongeza kwamba "mgogoro haupaswi kutekelezwa kwa migongo ya maskini zaidi kwenye sayari hii".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.