Pata taarifa kuu

G7 yaahidi msaada wa kijeshi wa muda mrefu kwa Ukraine ikisubiri Kyiv kujiunga na NATO

Mataifa yenye nguvu ya G7 yameahidi kutoa msaada wa kijeshi wa muda mrefu kwa Ukraine, hatua ambayo imeshangiliwa na rais Volodymyr Zelensky, ambaye hata hivyo amesisitiza kuwa hilo halipaswi kuchukua nafasi ya uanachama wa baadaye wa nchi yake katika Muungano huo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa amezungukwa na wakuu wa nchi na serikali wa nchi za G7 huko Vilnius mnamo Julai 12, 2023.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa amezungukwa na wakuu wa nchi na serikali wa nchi za G7 huko Vilnius mnamo Julai 12, 2023. AP - Pavel Golovkin
Matangazo ya kibiashara

Katika siku ya pili ya mkutano wa kilele wa NATO, siku ya Jumatano, katika mji mkuu wa Lithuania, Vilnius, na karibu miezi 18 baada ya kuanza kwa uvamizi wa Urusi, wanachama wa G7 (Marekani, Uingereza, Ufaransa, Canada, Ujerumani, Italia, Japan) waliwasilisha mpango kwa usalama wa Ukraine. Hii ni kuisaidia kukabiliana na mashambulizi ya sasa ya Urusi na kuizuia Urusi dhidi ya "shambulio lolote la siku zijazo la silaha" dhidi ya jirani yake.

Tangazo hili, ambalo liliikasirisha Moscow, lilielezewa na Volodymyr Zelensky kama "ushindi muhimu kwa usalama wa Ukraine." Lakini alichukua tahadhari kukumbuksha kwamba "dhamana bora kwa Ukraine ni kuwa katika NATO", baada ya kuwakashifu viongozi wa Muungano siku moja kabla ya kutoweka ratiba ya kuunganishwa kwa nchi yake na muungano huu baada ya vita kumalizika.

'Mustakabali wa Ukraine uko katika NATO'

"Mustakabali wa Ukraine uko katika NATO," Rais wa Marekani Joe Biden amehakikisha. Lakini, wakati huo huo, "tutawasaidia (Waukraine) kujenga uwezo mkubwa wa ulinzi juu ya nchi kavu, baharini na angani", amesema, kabla ya kusifu ujasiri wa nchi hii, mfano "kwa ulimwengu wote. ".

Azimio la G7 linatoa mfumo wa kuhitimisha baadae mikataba ya nchi mbili kati ya nchi wanachama wake na Kyiv inayoelezea kwa undani silaha watakazosambaza. Nchi zingine nane zimejiunga na mpango huu: Uhispania, Uholanzi, Ureno, Iceland, Norway, Denmark, Poland na Jamhuri ya Czech.

"Lazima tuhakikishe kwamba vita vinapoisha kunakuwa na mifumo ya kuaminika ya usalama wa Ukraine ili historia isijirudie", pia alisema Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, kabla ya mkutano wa kwanza wa "Baraza la Ukraine naNATO" pamoja  na Volodymyr Zelensky. "Leo tunakutana kama watu sawa na ninatazamia siku ambayo tutakutana kama washirika," aliongeza Jens Stoltenberg, ambaye ameteuliwa tena kwa mwaka mmoja kama mkuu wa NATO.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.