Pata taarifa kuu

Licha ya wito wa Zelensky, NATO yakatisha hamu Kyiv

Ukraine itajiunga na NATO mara tu masharti yatakapotimizwa, Jens Stoltenberg amesema Jumanne baada ya siku ya kwanza ya mkutano wa kilele wa NATO. Habari ambazo Rais Volodymyr Zelenski amepokea huko Vilnius ambako alikwenda kukutana na viongozi wa Lithuania.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa hotuba yake huko Vilnius mnamo Julai 11, 2023.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa hotuba yake huko Vilnius mnamo Julai 11, 2023. AFP - PETRAS MALUKAS
Matangazo ya kibiashara

Juu ya kujiunga kwa Ukraine katika jumuiya hii, viongozi wa nchi wanachama wa NATO wamekubaliana Jumanne kuialika Ukraine kujiunga na Muungano huu "wakati masharti yatakapotimizwa", kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg. Hakuna ratiba iliyowekwa.

Sio aina ya mwaliko ambao Ukraine na Rais wake Volodymyr Zelensky walikuwa wakitarajia, ambaye, muda mfupi kabla ya kuwasili kwake Lithuania, alielezea kuwa "upuuzi" ukweli kwamba nchi yake haikuwa na ratiba ya uanachama. "NATO itaipa Ukraine usalama. Ukraine itaifanya NATO kuwa na nguvu zaidi,” alisema Bw. Zelensky, ambaye alitarajia zaidi kutoka kwa washirika wa Magharibi.

Taarifa ya mwisho ya mkutano huo pia inaonyesha kuwa mustakabali wa Ukraine uko katika NATO. Ahadi kama hiyo ilikuwa tayari imetolewa kwenye mkutano wa kilele wa Bucharest mnamo 2008. Hata hivyo, leo, muktadha ni tofauti, anathibitisha mbunge wa Ukraine Oleksyi Haran, kwa sababu "Urusi katika vita ni shida ya NATO na ulimwengu wote huru", anaelezea mtu ambaye anajuta kwamba muunano wa transatlantic unashindwa kuchukua "maamuzi ya ujasiri".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.