Pata taarifa kuu

Mkutano wa wakuu wa nchi za NATO kuanza mjini Vilnius, Lithuania

Nchi ya Ukraine, imeendelea kuzishinikiza nchi wanachama za jumuiya ya NATO kulikubali taifa hilo kuwa mwanachama mpya, wakati huu wakuu wa nchi wakitarajiwa kuanza mkutano wao mjini Vilnius, Lithuania.

Wakuu wa nchi za NATO wanakutana mjini Vilnius, Lithuania
Wakuu wa nchi za NATO wanakutana mjini Vilnius, Lithuania © REUTERS - INTS KALNINS
Matangazo ya kibiashara

Kupitia ukurasa wa kijamii wa Twitter, rais Volodymry Zelensky, amesema ni muhumu maombi ya taifa hilo kuchukuliwa kwa umakini licha ya kuwa nchi kadhaa haziungi mkono ikiwemo Marekani.

‘‘Ukraine itashiriki mkutano wa NATO huko Vilnius, mkutano ambao huenda ukawa ni kile ambacho nchi yetu inataka, muungano wote na kwa usalama wa dunia, hivi karibuni tunafanya kazi sana kuliko kawaida licha kuwa kazi hii ni karibia asilimia 100 sio kwamba ni kazi muhimu kuliko kazi nyengine za umma, kila mtu anaelewa kil akitu.’’alisema rais Volodymry Zelensky.

00:38

Volodymry Zelensky, Rais wa Ukraine

Mkutano wa Vilnius, hata hivyo unatarajiwa kutoa muelekeo wa namna ombi la Ukraine litashughulikiwa kwa haraka.

Katika hatua nyengine, Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, hatimaye amekubali kuunga mkono maombi ya Sweden kuwa mwanachama mpya wa NATO, baada ya karibu mwaka mzima kwa kile Ankara imekuwa inazuia maombi hayo kwa sababu za kiusalama.

Katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, amesema hatua hii ni ya kihistoria.

‘‘Kukamilisha mchakato wa Sweden kuwa mwanachama wa NATO ni hatua ya kishtoria, ambayo ina manufaa ya kiusalama kwa nchi wanachama katika nyakati hizi.’’ alisema Jens Stoltenberg.

00:32

Jens Stoltenberg, Katibu mkuu wa NATO

Uturuki ilikuwa imeweka ngumu kwa Sweden kuwa mwanachama ikitaka kwanza taifa hilo kuwakabidhi wale iliowataja wahusika wa jaribio la mapinduzi na wafadhili wa matukio ya ugaidi nchini mwake na ambao wanapewa hifadhi Stolkhom.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.