Pata taarifa kuu

Vita vya Ukraine: Watatu wauawa na wengine kadhaa wajeruhiwa Lviv katika shambulio

Shambulio la kombora' limeua takriban watu watatu na 'miundombinu muhimu' huko Lviv, magharibi mwa Ukraine, mamlaka zandani zimeripoti mapema Alhamisi.

Urusi inaendelea kuruha makomora katika baadhi ya maeneo ya Ukraine.
Urusi inaendelea kuruha makomora katika baadhi ya maeneo ya Ukraine. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

"Watatu wameuawa," Andriï Sadovyi amesema katika ujumbe wa Telegraph, baada ya kuripoti "majeruhi wanane" na "vyumba vingi" vilivyoharibiwa kulingana na video, iliyotumwa pia kwenye mtandao wa kijamii.

Hapo awali, diwani wa jiji hilo aliripoti "msururu wa milipuko" iliyosikika jijini. "Kila kitu kimerejea katika hali ya kawaida (...) Huduma zote za manispaa zinafanya kazi bila wasiwasi," ameongeza afisa huyo aliyechaguliwa.

Mashambulizi kadhaa

Miundombinu muhimu pia imeharibiwa "kulingana na taarifa za awali", mkuu wa utawala wa kikanda Maksym Kozytskyi ameandika kwenye Telegraph, baada ya kuripoti mapema usiku kwamba "makombora kadhaa ya adui" yalikuwa yakielekea magharibi mwa nchi.

Kilomita mia kadhaa kutoka kwenye uwanja wa vita, Lviv na jimbo lake yamekuwa yakilengwa na mashambulizi mara kadhaa tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 24, 2022.

Usiku wa Juni 19 kuamkia 20, "miundombinu muhimu" huko Lviv ilishambuliwa na ndege zisizokuwa na rubani, Maksym Kozytskyi ameripoti. Watu watano waliuawa mnamo mwezi Machi kwa kupigwa risasi katika eneo la makazi la Velyka Vilchanytsia, katika jimbo la Lviv.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.