Pata taarifa kuu

Urusi yainyooshea lawama Kiev baada ya kuharibu ndege tano zisizo na rubani

Urusi imeshutumu 'kitendo cha kigaidi' kilichofanywa na Kyiv baada ya kudondosha ndege tano zisizo na rubani karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Moscow.

Ndege tano zisizo na rubani za Ukraine zimedondoshwa Jumanne, Julai 4, karibu na Moscow na vitongoji vyake lake, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Urusi.
Ndege tano zisizo na rubani za Ukraine zimedondoshwa Jumanne, Julai 4, karibu na Moscow na vitongoji vyake lake, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Urusi. AFP - NATALIA KOLESNIKOVA
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo, Jumanne hii, Julai 4, limelenga maeneo yaliyo karibu na mji wa Moscow na vitongoji yake, na shughuli mbalimbali katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Vnukovo.

"Leo asubuhi, tumezuia jaribio la serikali ya Kiev kutekeleza kitendo cha kigaidi kwa kutumia ndege tano zisizo na rubani", kitendo ambacho kumenga maeneo katika jimbo la Moscow na kando ya mji mkuu wa Urusi, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema katika taarifa. Ndege nne zisizo na rubani ziliharibiwa na mfumo wa ulinzi wa anga karibu na mji mkuu na ya tano iliangamizwa na "mfumo vita vya kielektroniki", kabla ya kuanguka katika jimbo la Moscow, kulingana na chanzo hicho.

Shambulio hilo halikusababisha hasara wala vifo, wizara ya ulinzi imesema. "Mashambulizi yote yalizuiliwa na mfumo ulinzi wa anga, ndege zote zisizo na rubani zilizogunduliwa ziliangamizwa," Meya wa Moscow Sergei Sobyanin amesema kwenye Telegraph.

Kulingana na idara ya huduma za dharura iliyonukuliwa na shirika la habari la umma la RIA Novosti, moja ya ndege zisizo na rubani ilidondoshwa karibu na Kubinka, eneo linalopatikana kilomita arobaini kutoka uwanja wa ndege wa Moscow wa Vnukovo, ambapo shughuli zilitatizwa kwa muda mfupi kutokana na shambulio hilo. Uwanja wa ndege wa Vnukovo, ambapo ndege kadhaa zilielekezwa kwenye viwanja vya ndege vingine asubuhi, "ulianza tena shughulizake" saa kumi Alfajiri saa za Afrika Mashariki, kulingana na Shirika la Usafiri wa Anga la Urusi (Rosaviatsia).

'Kitendo cha kigaidi'

Baada ya shambulio hilo, diplomasia ya Urusi ilishutumu "kitendo cha kigaidi" cha Kyiv. "Jaribio la serikali ya Kyiv kushambulia eneo ambalo maeneo ya miundombinu ya kiraia yanapatikana, pamoja na uwanja wa ndege ambao, hupokea ndege za kimataifa, ni kitendo kipya cha kigaidi," msemaji wa diplomasia ya Urusi, Maria Zakharova amesema kwenye Telegraph.

Kwa kuzingatia kwamba Rais wa Ukraine Volodymyr "Zelensky anafanya vitendo hivi vya kigaidi kwa kutumia silaha zinazotolewa na nchi za Magharibi au kununuliwa kwa ufadhili wa Magharibi, huu ni ugaidi wa kimataifa", amesema.

Mnamo tarehe 21 Juni, Urusi ilitangaza kuwa iliharibu ndege tatu zisizo na rubani katika eneo la mji mkuu wake, zikiwemo mbili karibu na kambi ya kijeshi, ikiituhumu Kyiv kuhusika naa shambulio hilo. Mwanzoni mwa mwezi Mei, ndege mbili zisizo na rubani zililenga Kremlin huko Moscow, na vifaa vingine viligonga majengo katika mji mkuu wa Urusi mwishoni mwa mwezi huo. Vikosi vya Ukraine vilianzisha operesheni kubwa mwanzoni mwa mwezi Juni ili kutwaa tena maeneo yaliyokuwa yakikaliwa na Urusi, lakini mafanikio yanabakia kuwa machache kwa sasa.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.