Pata taarifa kuu

Ukraine kumfungulia mashtaka mshukiwa wa shambulio la Kramatorsk

Nairobi – Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa mwanaume aliyakamatwa kwa tuhuma za kuelekeza makombora ya Urusi yaliolenga mgahawa mmoja katika mji wa Kramatorsk, na kusababisha vifo vya watu 11, na kujeruhi wengine zaidi ya 60, atashtakiwa kwa makosa ya uhaini.

Volodymyr Zelensky, Rais wa Ukraine
Volodymyr Zelensky, Rais wa Ukraine AP
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa usalama wa Ukraine walisema kuwa mwanamume aliyemkamata, mfanyakazi wa kampuni ya usafirishaji wa mafuta, alishukiwa kurekodi mgahawa huo kwa ajili ya wanajeshi wa Urusi na kuwafahamisha kuhusu umaarufu wake.

Ukraine inaithumu Urusi kwa kuhusika na shambulio katika mgahawa mjini  Kramatorsk
Ukraine inaithumu Urusi kwa kuhusika na shambulio katika mgahawa mjini Kramatorsk Β© Genya Savilov / AFP

Aidha akihutubia bunge hapo jana Jumatano, katika maadhimisho ya siku ya katiba, Zelensky ametupilia mbali mpango wowote wa amani ambao anasema unatageuza vita dhidi ya nchi yake kuwa mzozo ulioganda.

β€œUongozi wa kijeshi na kisiasa nchini Urusi haupaswi kukwepa haki kutokana na sababu kwamba inakinga ya viongozi wa serikali, wao sio viongozi wa serikali bali ni majambazi waliochukua uongozi wa taasisi ya serikali za Urusi.” alisema rais Zelensky.

00:23

Volodymyr Zelensky, Rais wa Ukraine

Idadi ya waliofariki kutokana na shambulio hilo iliongezeka hadi 12 siku ya Alhamisi kufuatia kugunduliwa kwa maiti nyingine, huduma za dharura za Ukraine zilisema.

Shambulio la kombora la Jumanne pia liliharibu majengo 18 ya orofa mbalimbali, nyumba 65, shule tano, shule mbili za chekechea, kituo cha ununuzi, jengo la utawala na jengo la burudani, Gavana wa mkoa wa Donetsk nchini Ukraine Pavlo Kyrylenko alisema.

Raia watatu wa Colombia pia walijeruhiwa katika shambulio hilo kwenye mgahawa huo, Rais wa Colombia Gustavo Petro alisema katika ujumbe wa Twitter siku ya Jumatano, akiongeza kwamba Bogota itafanya maandamano ya kidiplomasia dhidi ya Moscow kwa shambulio ambalo limewadhuru "raia wasio na ulinzi wa Colombia".

Raia watatu wa Colombia waliojeruhiwa walitambuliwa kama mwandishi mashuhuri Hector Abad Faciolince, msuluhishi wa zamani wa amani wa Colombia Sergio Jaramillo na mwanahabari Catalina Gomez.Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.