Pata taarifa kuu

Ukraine yadai kuendesha 'mapambano makali' dhidi ya jeshi la Urusi mashariki

Ukraine imekiri hivi punde kwamba vikosi vya Urusi vilikuwa vinasonga mbele katika maeneo manne ya uwanja wa vita mashariki ambako "mapigano makali" yanaripotiwa, lakini imehakikisha kwamba wanajeshi wake wanasonga mbele kusini, takriban mwezi mmoja baada ya kuanzishwa kwa mashambulizi yao.

Ukraine imekiri kwamba vikosi vya Urusi vinasonga mbele katika maeneo manne ya uwanja wa vita mashariki ambako "mapigano makali" yanaripotiwa.
Ukraine imekiri kwamba vikosi vya Urusi vinasonga mbele katika maeneo manne ya uwanja wa vita mashariki ambako "mapigano makali" yanaripotiwa. AFP - GENYA SAVILOV
Matangazo ya kibiashara

"Adui anasonga mbele katika maeneo ya Avdiivka, Mariinka, Lyman," Naibu Waziri wa Ulinzi Ganna Maliar ameandika kwenye Telegram. "Pia anaendelea katika eneo la Svatove". "Hali ni ngumu sana," ameongeza. "Kuna mapigano makali kila mahali."

Miezi kumi na sita baada ya kuanza kwa uvamizi wa Urusi, Ukraine inasema inaendelea na mashambulizi yake na ambayo yalizinduliwa takriban mwezi mmoja uliopita na ambayo hadi sasa yameshindwa kuleta maendeleo madhubuti, na kuwataka washirika wake wa Magharibi kuharakisha msaada wa kijeshi ulioahidiwa kuelekea mkutano wa kilele wa NATO huko Vilnius.

Wanajeshi wa Ukraine wasonga mbele kwa 'mafanikio madogo'

Matukio haya ya hivi punde kwenye uwanja wa vita yanakuja baada ya shambulio lingine la ndege isiyo na rubani usiku katika mji wa Kyiv, shambulio la kwanza katika kipindi cha siku 12, kulingana na maafisa wa Ukraine. "Ndege zote za adui katika anga karibu na Kiev yamegunduliwa na kuharibiwa," amesema Sergiy Popko, mkuu wa utawala wa kijeshi wa mji mkuu huo.

Jeshi la Wanahewa la Ukraine, katika taarifa tofauti, limesema kuwa limeangusha ndege nane za vilipuzi za Shahed zilizotengenezwa na Iran na makombora matatu. Amesema wanajeshi wa Ukraine wanasonga mbele kwa upande wao kwa "mafanikio madogo" kwenye eneo la kusini wa mji wa Bakhmut, mashariki, na vile vile karibu na Berdiansk na Melitopol katika ukanda wa kusini mwa uwanja wa vita.

Kwa upande wa kusini, alisema vikosi vya Ukraine vilikuwa vikikabiliana na "upinzani mkubwa wa adui" pamoja na maeneo ya migodi, na walikuwa wakisonga mbele "hatua kwa hatua". Wanajeshi wa Ukraine "wanafanya kazi kwa kuendelea na bila kuchoka kuunda mazingira ya haraka iwezekanavyo", ameandika tena.

Kyiv inabaini ukosefu wa silaha na mafunzo ya marubani

Kamanda mkuu wa jeshi la Ukraine Valery Zalouzhny alibaini, katika mahojiano yaliyochapishwa Ijumaa na Gazeti laWashington Post, kwamba vikosi vya Kyiv vinakabiliwa na ukosefu wa silaha. Alikuwa ametaka hasa kutumwa kwa ndege za kivita za Marekani F-16, muhimu ili kukabiliana na jeshi la anga la Urusi. 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, akimpokea Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez siku ya Jumamosi, wakati huo huo alikosoa washirika wa Magharibi wa Kiev juu ya kasi ya utekelezaji wa mafunzo ya marubani wa Ukraine, waliozoea kuendesha ndege aina ya MiGs na Sukhoi za Sovieti ya zamani.

Mkuu wa majeshi wa Marekani Mark Milley, kutoka Washington, alijibu kwamba Marekani na washirika wake wanafanya wawezavyo kutuma kile Ukraine inahitaji. Uwasilishaji wa ndege F-16 au makombora ya ATACMS  "uko mezani, lakini bado hakuna uamuzi ambao umechukuliwa," amesema. Mashambulizi ya Ukraine "yanakwenda polepole kuliko tulivyotabiri", ameongeza, lakini "vita ndivyo hivyo".

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.