Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Zelensky aonya dhidi ya 'chokochoko' kwenye kituo Zaporizhia

Rais wa Ukraine amemfahamisha rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuhusu uwezekano wa kutokea shambulizi kutoka Urusi. Vifaa vya kulipuka viliwekwa kwenye kituo cha nyukilia cha Zaporizhia.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, huko Kyiv, Ukraine, Julai 1, 2023.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, huko Kyiv, Ukraine, Julai 1, 2023. © Sergei CHUZAVKOV / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mvutano mpya unaripotiwa karibu na kituo cha nyuklia cha Zaporizhia. Jumanne hii, Kyiv iliishutumu Moscow kwa kuchochea "uhasama" katika kinu cha nyuklia kilichoko kusini mwa Ukraine. Jengo hilo linashikiliwa na askari wa Urusi. Urusi, kwa upande wake, inadai kwamba Ukraine inaandaa "mashambulizi" kwenye mitambo ya kituo hiki.

Jeshi la Ukraine lilionya juu ya "maandalizi ya uwezekano wa uchochezi kwenye eneo la kituo cha nyuklia cha Zaporizhia katika siku za usoni". Onyo lilitolewa katika simu Volodymyr Zelensky aliyompigia rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Jumanne jioni. Ukraine inaona kwamba "vitu sawa na vifaa vya vilipuzi viliwekwa kwenye paa la nje la kinu cha 3 na cha 4".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.