Pata taarifa kuu

Ghasia Ufaransa: Macron kupokea viongozi kutoka ngazi mbalimbali

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atawapokea leo Jumatatu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Yaël Braun-Pivet, na rais wa Bunge la Seneti, Gérard Larcher, kisha siku ya Jumanne mameya wa "zaidi ya manispaa 220 waathiriwa wa dhuluma" wakati wa ghasia za hivi karibuni, ikulu ya Elysée ilitangaza Jumapili jioni. "Rais pia alimwomba Waziri Mkuu Elisabeth Borne kupokea marais wa makundi ya kisiasa katika Bunge siku ya Jumatatu," ikulu ya rais iliongeza.

Emmanuel Macron atawapokea marais wa Bunge la Kitaifa na Seneti siku ya Jumatatu, kisha Jumanne mameya wa "zaidi ya manispaa 220 waathiriwa wa dhuluma" wakati wa ghasia za siku chache zilizopita.
Emmanuel Macron atawapokea marais wa Bunge la Kitaifa na Seneti siku ya Jumatatu, kisha Jumanne mameya wa "zaidi ya manispaa 220 waathiriwa wa dhuluma" wakati wa ghasia za siku chache zilizopita. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron "anataka kuanza kazi ya uangalifu na ya muda mrefu ili kuelewa kwa kina sababu zilizosababisha matukio haya", Élysée imebainisha.

"Ni lazima kwanza tukariri matukio haya kabla ya kufanya hitimisho," alisisitiza rais wa Ufaransa, kulingana na mmoja wa washiriki, wakati wa mkutano na kiongozi wa serikali na mawaziri sita, ikiwa ni pamoja na Gérald Darmanin - Waziri wa Mambo ya Ndani - na Eric Dupond-Moretti - Waziri wa Sheria -, Jumapili jioni katika ikulu ya Élysée.

Rais Macron pia amewataka mawaziri "kuendelea kuwepo uwanjani, kila mmoja katika eneo lake ilikutathmini hali ya mambo", imeelezwa. Ataongoza mkutano mpya katika muundo kama huo "ndani ya kipindi cha saa 48" ili kutathmini hali hiyo.

Emmanuel Macron pia aliwataka mawaziri wake "kuendelea kufanya kila kitu kurejesha utulivu na kuhakikisha kurejea kwa utulivu", mmoja wa washiri katika mkutano huo ameongeza. "Pia aliiomba serikali kuendelea kuwa pamoja na polisi, askari, mahakimu, makarani, maafisa aw Zima moto, viongozi waliochaguliwa".

Wabunge wa walio wengi hasa wamealikwa kushiriki katika mikutano ya kuwaunga mkono viongozi waliochaguliwa iliyoandaliwa Jumatatu saa sita mchana mbele ya kumbi za miji kote Ufaransa.

Kulingana na chanzo cha serikali, "bado hatujatoka katika hali hii na lazima tuendelee kuangazia hali itakavyokuwa katika saa zijazo". Lazima "tuonyeshe umoja wa taifa", pia alisisitiza Emmanuel Macron.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.