Pata taarifa kuu

Machafuko nchini Ufaransa: 'Njia za ziada' zitatumika, atangaza Macron

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amelaani leo Ijumaa 'watu kutumia kifo cha Nahel ni jambo lisilokubalika' na akatangaza kwamba 'njia za ziada' zitatumiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani baada ya usiku wa tatu wa ghasia za mijini kufuatia kifo cha kijana Nahel wakati wa ukaguzi wa magari barabarani, tukio lililotokea huko Nanterre.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza kufuatia mkutano wa dharura wa serikali baada ya ghasia kuzuka kwa usiku wa tatu mfululizo nchini humo, katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani huko Paris, Ijumaa, Juni 30, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza kufuatia mkutano wa dharura wa serikali baada ya ghasia kuzuka kwa usiku wa tatu mfululizo nchini humo, katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani huko Paris, Ijumaa, Juni 30, 2023. AP - Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa Kamati ya Mgogoro ya Mawaziri iliyofanyika katika Wizara ya Mambo ya Ndani, rais Emmanuel Macron amekaribisha jibu la "haraka na linalofaa" kutoka kwa polisi. Pia amewaita "wazazi wote kuwajibika" na pia ameomba mitandao ya kijamii "kuondoa" maudhui na kutambua watumiaji wanaohusishwa na vurugu hizi za mijini.

Alhamisi asubuhi, rais aliitisha mkutano wa kwanza wa kutatua mgogoro na mawaziri na wakurugenzi wa utawala wanaohusika, katika kituo cha dharura kilichopo katika Wizara ya Mambo ya Ndani, kabla ya kuondoka kuelekea Brussels. Alishutumu ghasia "zisizo halali".

Taarifa zaidi zinakujia...

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.