Pata taarifa kuu

Ufaransa: Vurugu zapungua mijini, nyumba ya meya yashambuliwa kwa gari

Baada ya usiku wa nne wa vurugu za mijini kote Ufaransa kufuatia kifo cha Nahel huko Nanterre, aliyeuawa Jumanne Juni 27 wakati wa ukaguzi wa magari barabarani huko Nanterre, katika vitongoji vya Paris, usiku wa Jumamosi Julai 1 hadi Jumapili Julai 2 ulikuwa shwari, saa chache baada ya mazishi ya kijana huyo.

Huko Paris,idadi kubwa ya vikosi vya usalama ilitumwa Jumamosi jioni kando ya Champs-Élysées, ambapo wito wa kuwataka raia kukusanyika zilikuwa zikizunguka kwenye mitandao ya kijamii.
Huko Paris,idadi kubwa ya vikosi vya usalama ilitumwa Jumamosi jioni kando ya Champs-Élysées, ambapo wito wa kuwataka raia kukusanyika zilikuwa zikizunguka kwenye mitandao ya kijamii. REUTERS - JUAN MEDINA
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya Ndani ilitangaza kukamatwa kwa watu 719. Katika L'Haÿ-les-Roses (Val-de-Marne), hata hivyo, nyumba ya meya wa jiji ilishambuliwa kwa gari, kulingana na Halmashauri ya wilaya.

"Usiku ulikuwa tulivu kutokana na hatua thabiti ya polisi," Gérald Darmanin ameonyesha furaha yake kwenye ukurasa wake wa Twitter. Kwa usiku wa pili mfululizo, waziri wa Mambo ya Ndani aliongeza idadi ya maafisa polisi na askari 45,000, ikiwa ni pamoja na 7,000 huko Paris na vitongoji vyake. Kufikia sasa, maafisa polisi 45 na askari wamejeruhiwa, magari 577 na majengo 74 yamechomwa moto, wakati visa 871 vya moto vimerekodiwa kwenye barabara za umma, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema.

Hata hivyo, katika mkoa wa Paris, nyumba ya meya wa mji mdogo wa L'Haÿ-les-Roses, karibu na mji wa Paris, ilishambuliwa kwa gari, kulingana na vyanzo kutoka Halmashauri ya wilaya. Karibu saa saba na nusu 30 usiku, wakati Meya Vincent Jeanbrun (LR, mengo wa kulia) alipokuwa katika makao makuu ya jiji lake, kundi la wahalifu lilishambilia kwa gari makazi yake kabla ya kulichoma moto,” alisema kwenye taarifa iliyochapishwa kwenye Twitter. Mkewe na mmoja wa watoto wake wawili wadogo "walijeruhiwa", aliongeza, akishutumu "jaribio la mauaji ya kikatili yasiyoelezeka". Polisi imeanzisha uchunguzi, kwa mujibu waofisi ya mashtaka.

Huko Nanterre, ambapo saa chache mapema, maelfu ya watu walihudhuria mazishi ya Nahel, kijana huyu mwenye umri wa miaka 17 aliyeuawa na afisa wa polisi wakati wa ukaguzi wa magari barabarani alipofyatuliwa risasi baada ya kukataa kutii amri ya kusimama, hali ilikuwa shwari. Usiku ulipoingia, hapakuwa na watu mitaani.

Matukio machache huko Marseille

Idadi kubwa ya polisi na vikosi vya jeshi vilitumwa huko Marseille na Lyon, miji mikubwa iliayothiriwa siku moja kabla na makabiliano, uharibifu au uporaji. Matukio machache yaliripotiwa katika miji hii miwili. 

Saa nane mchana, Wizara ya Mambo ya Ndani haikuwa imetambua matukio yoyote makubwa na iliripoti watu 719 waliokamatwa kote nchini.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.