Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Uasi wa Wagner: Beijing 'yaunga mkono' Moscow, kulingana na diplomasia ya Urusi

Urusi imesema Jumapili Juni 25 kwamba China imeeleza 'kuunga mkono' juhudi za Rais Vladimir Putin za "kurejesha hali ya nchi kuwa shwari" baada ya uasi wa kundi la wanamgambo la Wagner, ambaoo uliishtua Kremlin, limeandika shirika la habari la AFP.

Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) na kiongozi wa kundi la wanamgambo la Wagner Yevgeny Prigozhin.
Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) na kiongozi wa kundi la wanamgambo la Wagner Yevgeny Prigozhin. AFP - GAVRIIL GRIGOROV,SERGEI ILNITSKY
Matangazo ya kibiashara

Mamluki wa kampuni binafsi ya kijeshi ya Wagner wameanza siku ya Jumapili kurejea kwenye kambi zao baada ya kiongozi wao Yevgeny Prigozhin kukubali kwenda uhamishoni nchini Belarus.

Hatua hiyo inafuatia hatua ya Rais Vladmir Putin kuafiki makubaliano ya kutoa msamaha. Makubaliano hayo yanaonekana kukomesha mara moja tishio la Yevgeny kuwa jeshi lake lingeweza kuuvamima mji wa Moscow. Hata hivyo wachambuzi wanasema kuwa uasi wa Wagnerumeonesha udhaifu katika utawala wa Putin.

Kwa upande mwingine Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amekuwa akizungumza kuhusu hali nchini Urusi.

Blinken anasema uasi wa muda mfupi kutoka kwa mamluki wa Wagner unaonyesha "mpasuko halisi" katika mamlaka ya Putin, kulingana na shirika la habari la AFP.

Uasi wa kundi la kibinafsi la mamluki na kiongozi wake Yevgeny Prigozhin mwishoni mwa juma ulikuwa "pingamizi ya moja kwa moja kwa mamlaka ya Putin", Blinken amesema.

"Kwa hivyo hii inazua maswali mazito, inaonyesha mpasuko halisi," Blinken aliambia kipindi cha mazungumzo cha CBS News 'Face the Nation'.

Ni mapema mno kusema nini mustakabali wa kundi la mamluki la Wagner walioasi jana, Blinken anasema.

Kama tumekuwa tukiripoti, Kremlin imesema haitowafungulia mashtaka wanajeshi wa Wagner ambao waliasi jana, licha ya kuwashutumu mapema kwa uasi wa kutumia silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.