Pata taarifa kuu

Macron: Uasi wa Wagner dhidi ya Putin unaonyesha 'migawanyiko iliyopo' nchini Urusi

Baada ya uasi waYevgeny Prigozhin na wanamgambo wake wa Kundi la Wagner nchini Urusi, Emmanuel Macron amesema mgogoro wa ghafla nchini humo umeonyesha "migawanyiko iliyopo ndani ya kambi ya Urusi", katika mahojiano na gazeti la La Provence, Jumapili hii, Juni 25.

Rais wa Urusi Vladimir Putin wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya Kremlin huko Moscow mnamo Juni 13, 2023.
Rais wa Urusi Vladimir Putin wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya Kremlin huko Moscow mnamo Juni 13, 2023. © AP/Gavriil Grigorov
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa, ambaye anadai kuwa "Alikuwa akifuata matukio saa baada ya saa, kwa kushirikiana na washirika wakuu wa Ufaransa" anaona kwamba hali hiyo imeonyesha udhaifu wa majeshi ya Urusi, pamoja na ule "wa vikosi washirika wa jeshi la Urusi, kama vile kundi la Wagner.

Akirejelea hali "ambayo imeanza kuwa shwari", Emmanuel Macron amebaini kwamba "yote haya (yanapaswa) kutufanya tuwe macho sana na (kuhalalisha) uungwaji mkono kamili tunaowapa Waukraine katika ukakamavu wao dhdi ya uvamizi wa Urusi. "

Mpasuko mkubwa unaripotiwa katika ngazi ya juu ya nchi, kulingana na Washington

Siku ya Jumapili, Marekani pia imebaini kwamba uasi wa Wagner uliyositishwa ulikwenda kinyume na mamlaka ya rais wa Urusi Vladimir Putin, na hivyo kufichua "nyufa" katika ngazi ya juu ya nchi na hivyo kulazimika "kuuhami" mji wa Moscow, kulingana na maneno ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken.

Jumamosi Juni 24, wanajeshi wa Urusi na wanamgambo wa Wagner walikabiliana kufuatia mwito wa uasi uliotolewa na mwanzilishi wa kundi hili la wanamgambo, Yevgeny Prigozhin. Alikuwa ameahidi kutuma askari wake huko Moscow, kabla ya kujirudi mapema alaasiri, akiwataka askari wake kurejea kambini kwa kuepuka umwagikaji wa damu.

Hasira zamkuu wa Wagner, mshirika wa muda mrefu wa Vladimir Putin, zilichochewa na shambulio la jeshi la Urusi ambalo lilidaiwa kuua "idadi kubwa" ya wanajeshi wake katika shambulio la anga nyuma ya uwanja wa vita dhidi ya Ukraine. Madai yaliyokanushwa na Moscow, ambayo ilitangaza kuwa Yevgeny Prigozhin, hatashtakiwa, na atakwenda uhamishoni nchini Belarus hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.