Pata taarifa kuu

Uingereza: Masaibu yaendelea kumwandama waziri mkuu wa zamani Boris

NAIROBI – Kamati ya Bunge nchini Uingereza imesema Waziri Mkuu wa zamani Boris Johnson, kwa makusudi, aliwadanganya wabunge kuhusu hatua yake ya kwenda kinyume na masharti ya kutokutana na watu, wakati Ofisi yake ilipoandaa sherehe kipindi cha maambukizi ya janga la Uviko 19.  

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Boris Johnson, London, Uingereza, Machi 21, 2023.
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Boris Johnson, London, Uingereza, Machi 21, 2023. © REUTERS / PETER NICHOLLS
Matangazo ya kibiashara

Kamati hiyo ya Bunge inayochunguza iwapo wabunge wamevunja kanuni na taratibu za Bunge, katika ripoti yake ya kurasa 106, imesema hatua ya Boris kusema uongo mbele ya Bunge inasikitisha hasa kutoka kwa mtu wa kiwango chake ambaye alikuwa Waziri Mkuu.  

Boris ambaye siku chache zilizopita, alijiuzulu pia ubunge, anashtumiwa kwa kuwapotosha wabunge mara kadhaa.  

Hatua yake ya kujiuzulu inaelezwa kama njia ya kuepuka aibu mbele ya wabunge wenzake baada ya kubaini kuwa ripoti hiyo ilikuwa imempata na kosa.  

Wakati akijiuzulu Ijumaa iliyopita, Boris alisema aliamua kuachia nafasi hiyo kwa kile alichokieleza kuwa hawezi kupata haki, kutokana na kashfa hiyo inayomkabili aliyosema imetumiwa kisiasa, kumchafulia jina.  

Aidha, Boris katika taarifa yake, aliendelea kutetea uamuzi wake wa kuhudhuiria sherehe hizo akisema, ilikuwa sehemu ya kazi kama Waziri Mkuu.  

Katika ripoti hiyo ya Bunge, imependekezwa kuwa Boris apokonywe utambulisho kama mbunge wa zamani, uamuzi ambao utaamuliwa na wabunge Jumatatu ijayo, wakati watakapopiga kura.  

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.