Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Mji wa Zelensky wakumbwa na mashambulizi ya Urusi, ndege zisizo na rubani 20 zadunguliwa

Ukraine imetangaza kuwa imeharibu ndege 20 za vilipuzi zilizotumwa na Urusi. Tatu kati ya ndege hizo zimeshambulia mji alikozaliwa rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Mashambulizi haya ya Ukraine yanalenga kurudisha nyuma vikosi vya Urusi kutoka maeneo wanayomiliki Kusini na Mashariki. Mamlaka ya Ukraine imebaini kuwa inakusudia kutwaa tena maeneo yote, ikiwa ni pamoja na Crimea na maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa watu wanaounga mkono Urusi kujitenga tangu mwaka wa 2014.
Mashambulizi haya ya Ukraine yanalenga kurudisha nyuma vikosi vya Urusi kutoka maeneo wanayomiliki Kusini na Mashariki. Mamlaka ya Ukraine imebaini kuwa inakusudia kutwaa tena maeneo yote, ikiwa ni pamoja na Crimea na maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa watu wanaounga mkono Urusi kujitenga tangu mwaka wa 2014. AFP - ANATOLII STEPANOV
Matangazo ya kibiashara

Mji alikozaliwa Rais Volodymyr Zelensky ulikumbwa na mashambulizi ya makombora matatu yaliyotumwa na Urusi usiku wa Jumatano Juni 14 kuamkia Alhamisi Juni 15, 2023. Ukraine, kwa upande mwingine, imetangaza kuwa imetungua kombora la cruise na ndege zisizo na rubani 20 za Urusi. Kwa mujibu wa habari zilizotumwa na Jeshi la Wanahewa la Ukraine, ndege hizo 20 zisizo na rubani zilizorushwa kutoka Kaskazini na Kusini pamoja na moja ya makombora manne ya Cruise yaliyorushwa kutoka Bahari ya Caspian yalinaswa.

Makombora mengine matatu yameanguka katika "mitambo ya viwanda katika mkoa wa Dnipropetrovsk", katikati mwa nchi hiyo, limemeongeza jeshi hilo kwenye Telegram. Kwa mujibu wa mamlaka katika mkoa huo, ni mji wa Kryvyï Rig, alikozaliwa Rais Volodymyr Zelensky, ambapo yaliendeshwa mashambulizi ya awali ya Urusi siku ya Jumanne na kusababisha vifo vya watu 12, na kuharibu jengo la ghorofa na ghala.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 58 auawa

"Makombora matatu yalipiga makampuni mawili ya viwanda ambayo hayana uhusiano wowote na jeshi," mkuu wa utawala wa kijeshi wa jiji hilo, Oleksandre Vilkoul, amesema kwenye Telegram. Mwanamume mwenye umri wa miaka 38 alijeruhiwa na kulazwa hospitalini, lakini maisha yake hayako hatarini, ameongeza. Katika eneo la Zaporizhia (kusini), maeneo 17 yalikumbwa na mashambulizi ya anga ya Urusi ambayo yameua mwanamke mwenye umri wa miaka 58 katika kijiji kimoja, utawala wa kikanda umesema kwenye Telegram siku ya Alhamisi.

Jiji la Kharkiv (kaskazini mashariki) na eneo la Odessa (kusini) pia zilishambuliwa wakati wa usiku na ndege zisizo na rubani za Urusi, ambazo zote zilidondoshwa, kulingana na mamlaka husika ya eneo hilo. Mapema siku hiyo, gavana huyo aliyewekwa na Moscow katika rasi ya Crimea, iliyotwaliwa mwaka 2014, alisema kuwa vikosi vya Urusi viliangusha ndege tisa zisizo na rubani za Ukraine kwenye eneo lake, jambo ambalo halikusababisha hasara yoyote.

Hata hivyo, ndege isiyo na rubani, iligonga kijiji kimoja katikati mwa peninsula, na kuvunja madirisha ya nyumba kadhaa. Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani huko Crimea, ambayo unyakuzi wake na Moscow haujatambuliwa na jumuiya ya kimataifa, na katika eneo la Urusi yameongezeka katika wiki za hivi karibuni wakati Ukraine imeanza mashambulizi kababme kenye uwanja wa vita.

Mashambulizi haya ya Ukraine yanalenga kurudisha nyuma vikosi vya Urusi kutoka maeneo wanayomiliki Kusini na Mashariki. Mamlaka ya Ukraine imebaini kuwa inakusudia kutwaa tena maeneo yote, ikiwa ni pamoja na Crimea na maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa watu wanaounga mkono Urusi kujitenga tangu mwaka wa 2014. Ukraine ilidai kupata faida ndogo kwa kutangaza kutekwa kwa vijiji vichache, baada ya zaidi ya wiki moja ya mapigano.

Urusi kwa upande wake imesema imevizuia vikosi vya Kyiv na kuzidisha mashambulizi ya usiku dhidi ya miji mikubwa ya Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.