Pata taarifa kuu

Ukraine: Mashambulizi ya mabomu yaathiri zoezi la kuwaondoa raia kwenye mafuriko

Mashambulizi ya maomu ya Urusi yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 18 na wengine 18 kujeruhiwa siku ya Alhamisi (tarehe 8 Juni) katika operesheni ya uokoaji katika mji wa Kherson uliokumbwa na mafuriko kusini mwa Ukraine, mamlaka ya Ukraine imeshutumu.

Wafanyakazi wa kujitolea wa shirika la Msalaba Mwekundu nchini Ukraine wakimuokoa mwanamke katika wilaya iliyokumbwa na mafuriko huko Kherson mnamo Juni 8, 2023, huku mamlaka ya Ukraine ikishutumu vikosi vya Urusi kwa kufanya mashambulizi ya mabomu katikati mwa zoezi la kuwaondoa raia kwenye mafuriko.
Wafanyakazi wa kujitolea wa shirika la Msalaba Mwekundu nchini Ukraine wakimuokoa mwanamke katika wilaya iliyokumbwa na mafuriko huko Kherson mnamo Juni 8, 2023, huku mamlaka ya Ukraine ikishutumu vikosi vya Urusi kwa kufanya mashambulizi ya mabomu katikati mwa zoezi la kuwaondoa raia kwenye mafuriko. © Evgeniy Maloletka / AP
Matangazo ya kibiashara

Ukraine na Urusi zimetupiana lawama, kila upande ukiutuhumu mwingine kuwashambulia watu wanaoondolewa katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko katika mkoa wa Kherson.

Mashambulizi hayo yamekuja saa chache baada ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuutembelea mji huo. Kwa upande wake, Urusi pia ilishutumu jeshi la Ukraine kwa mashambulizi mabaya, ikidai kuwa imerudisha nyuma shambulizi la vikosi vya Ukraine vilivyokuwa vilijihami kwa mbunduki za kivita ikiwa ni pamoja na vifaru kaskazini mwa nchi.

Raia wa Ukraine wamelishutumu jeshi la Urusi kwa kushambulia mji wa Kherson katika siku za hivi karibuni huku maelfu ya raia wakihamishwa kutoka maeneo yaliyokumbwa namafuriko kufuatia uharibifu wa bwawa la Kakhovka, lililoko juu ya mto Dnieper. Kulingana na Kyiv, mtu mmoja aliuawa na 18 kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na maafisa wa idara za huduma za dharura, katika mashambulizi ya anga ya Urusi katikati ya mji wa Kherson na eneo jirani.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametembelea eneo lililoathirika, na kuiomba jumuiya ya kimataifa kuwasaidia raia walio katika sehemu zinazokaliwa na Urusi. Mamia ya watu katika jimbo hilo hawana maji ya kunywa, hali iliyolilazimu jeshi la Ukraine kutumia ndege zisizo na rubani kuondosha maji ya chupa kwa watu wake walio na mahitaji. Hakuna upande huru uliothibitisha madai ya Urusi wala ya Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.