Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Zelensky: Sihusiki katika mlipuko wa bomba la gesi la Nord Stream

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekanusha kwamba hajahusika katika mlipuko wa bomba la gesi la Nord Stream na haamini kuwa maafisa wengine wa Ukraine wanahusika, kama magazeti kadhaa yalivyodai.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekanusha kwamba hajahusika katika mlipuko wa bomba la gesi la Nord Stream.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekanusha kwamba hajahusika katika mlipuko wa bomba la gesi la Nord Stream. AFP - BRENDAN SMIALOWSKI
Matangazo ya kibiashara

"Sijafanya jambo kama hilo, na sintothubutu kulifanya," amesema rais wa Ukraine katika mahojiano na vyombo vya habari vya Ujerumani vya Welt-TV na Bild ambayvyo vilimhoji kuhusu mazingira ya mlipuko wa bomba la gesi.

"Sidhani kama jeshi letu na idara zetu za ujasusi zimefanya kitu kama hicho, vinginevyo ningependa kuona ushahidi, hatujui chochote kati ya haya, kwa asilimia mia moja," ameongeza.

'Wahusika wangetafutwa nchini Ukraine'

Kwa mujibu wa makala ya Gazeti la Washington Post yaliyochapishwa siku ya Jumanne, shirika la kijasusi kutoka nchi ya Ulaya liliionya CIA mnamo mwezi Juni 2022 kwamba vikosi maalum vya Ukraine vinapanga kulipua bomba la gesi la Nord Stream. Gazeti la kila siku linanukuu taarifa kutoka kwa nyaraka nyingi za siri zilizochapishwa mtandaoni na mwanajeshi kijana wa Marekani Jack Teixeira aliyekamatwa katikati ya mwezi Aprili.

Kabla ya habari hii ya Gazeti la Washington Post, utafiti wa vyombo vya habari vya Ujerumani ulidai kuwa ushahidi mwingi juu ya hujuma ya mabomba ya gesi unaitaja Ukraine.

Vidokezo kadhaa "vinakubaliana na makadirio ya idara kadhaa za kijasusi, kwamba wahusika wangetafutwa nchini Ukraine", aliandika Spiegel mwishoni mwa mwezi Mei, akihoji ikiwa baadhi ya maafisa wa serikali ya Ukraine walifahamu hilo.

Nchi kadhaa zikiwemo Urusi, Ukraine na Marekani zimetuhumiwa kuanzisha hujuma hiyo lakini zote zimekanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.