Pata taarifa kuu

Ukraine: Zoezi la uokoaji laendelea baada ya uharibifu wa bwawa la Kakhovka

Zoezi la kuhamisha wa watu wengi linaendelea Jumatano hii, Juni 7 kusini mwa Ukraine baada ya uharibifu wa sehemu ya bwawa la Kakhovka, ambalo limsababisha mafuriko katika maeneo mengi kando ya Dnieper na ambayo Moscow na Kiev zinashumiana kwa kitendo hiki kiovu.

Bwawa la Kakhova, baada ya kuharibiwa mnamo Juni 6, 2023.
Bwawa la Kakhova, baada ya kuharibiwa mnamo Juni 6, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

"Hali ngumu zaidi iko katika wilaya ya Korabelny ya jiji la Kherson. Kufikia sasa, kiwango cha maji kimeongezeka kwa mita 3.5, zaidi ya nyumba 1,000 zimejaa mafuriko ", katika jiji hili lililochukuliwa kutoka na Ukraine kutoka mikononi mwa Urusi mnamo mwezi Novemba 2022, alisema katika taarifa kwa vyombo vya habari naibu mkurugenzi wa ofisi ya rais wa Ukraine, Oleksiï Kouléba. Zoezi la uokoaji litaendelea Jumatano na katika siku zijazo kwa basi na treni, amesema.

“Zaidi ya watu 40,000 wako katika hatari ya kuwa katika maeneo yenye mafuriko. Mamlaka ya Ukraine inawahamisha zaidi ya watu 17,000. Kwa bahati mbaya, zaidi ya raia 25,000 wako katika eneo lililo chini ya udhibiti wa Urusi," Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Ukraine Andriy Kostin alitangaza siku ya Jumanne.

"Katika hatua hii, maeneo ishirini na nne nchini Ukraine yamekumbwa na mafuriko," Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine Igor Klymenko amesema. Mamlaka zilizowekwa na Urusi katika mikoa wanayoishi zimesema zilikuwa zimeanza kuwahamisha wakazi wa maeneo matatu, baada ya kutuma karibu mabasi hamsini. Vladimir Leontiev, meya wa Nova Kakhovka aliyeteuliwa na Moscow, ambapo bwawa hilo linapatikana, almeema mji wake ulikuwa chini ya maji na wakaazi wake 900 wamehamishwa.

Moscow na Kyiv wanaendelea kushtumiana 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliishutumu Urusi kwa "kulipua bomu" kwenye bwawa hilo. 

"Ulimwengu lazima uchukue hatua. Urusi iko katika vita dhidi ya maisha, dhidi ya asili, dhidi ya ustaarabu", amesisitiza Volodymyr Zelensky, akihakikishia hata hivyo kwamba hii "haitaathiri uwezo wa Ukraine wa kukomboa maeneo yake".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.