Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Mmoja auawa, 22 wajeruhiwa katika shambulio la anga la Urusi Dnipro

Msichana wa miaka miwili ameuawa siku ya Jumapili katika shambulio la anga la Urusi katika mji wa Dnipro katikati mwa Ukraine. Takriban watu 22 wamejeruhiwa.

Waokoaji wakisimama kwenye vifusi vya jengo baada ya shambulio la anga la Urusi katika jiji la Dnipro, Ukraine.
Waokoaji wakisimama kwenye vifusi vya jengo baada ya shambulio la anga la Urusi katika jiji la Dnipro, Ukraine. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Urusi, kwa kushambulia jiji la Dnipro, imetaka "kushambulia mji huo". Ameongeza kuwa waathiriwa wengine walipatikana Jumapili hii chini ya vifusi vya majengo mawili ya makazi ambayo yaliporomoka kufuatia shambulio hilo.

"Usiku wa Jumamosi kuamkia leo Jumapili, mwili wa msichana huyo ulitolewa kutoka kwa vifusi vya nyumba" katika wilaya ya Pidhorodnenska, "alikuwa ametimiza miaka miwili," ameandika kwenye Telegram. Aidha, "watu 22 wamejeruhiwa, wakiwemo watoto watano," ameongeza katika ripoti yake ya hivi punde.

Shambulio hilo linakuja, huku mashambulizi ya anga yakizidi kushika kasi nchini Ukraine katika wiki za hivi karibuni. Huko Kyiv, mkuu wa utawala wa kijeshi wa eneo hilo amesema mfumo wa ulinzi wa anga wa mji mkuu ulizuia makombora na ndege zisizo na rubani usiku wa kuamkia leo Jumapili. "Kulingana na taarifa za awali, hakuna bomu lolote lililoanguka katika mji mkuu," Serhiy Popko ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram siku ya Jumapili.

Siku ya Jumapili, uwanja mdogo wa ndege pia ulilengwa na shambulio karibu na mji wa Kropyvnytskyi katikati mwa Ukraine, Jeshi la Wanahewa la Ukraine limesema. "Makombora sita na ndege zisizo na rubani tano" zilirushwa na vikosi vya Urusi, msemaji wa jeshi la wanahewa la Ukraine Yuriy Ignat amesema kwenye televisheni. "Kati ya makombora hayo sita), manne yaliharibiwa na mfumo wa ulinzi wa anga na mawili yalianguka katika uwanja mdogo wa ndege karibu na Kropyvnytskyi," ameongeza.

Mashambulio dhidi ya Urusi

Mashambulizi haya pia yanakuja huku Kyiv ikidai kuwa iko tayari kufanya mashambulizi dhidi ya ngome za Urusi mashariki mwa nchi na kubaini kwamba idadi ya wanajeshi wa Ukraine katika ardhi ya Urusi inazidi kuongezeka.

Gavana wa eneo hilo Vyacheslav Gladkov amesema kuwa watu wawili waliuawa kwa risasi Jumamosi huko Belgorod, Urusi. Vijiji vya mpakani katika eneo hili vimekumbwa na mashambulizi makubwa ambay hayajawahi kushuhudiwa katika siku za hivi karibuni, na kuua jumla ya watu saba wiki hii, kulingana na vyanzo vya Urusi.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.