Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Zelensky: Urusi 'inaitisha Ukraine' kwa mashambulizi ya usiku na ndege 36 zimedunguliwa

Urusi "inaendelea kutia hofu Ukraine" na mashambulizi yake ya usiku, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameshutumu Alhamisi, akitangaza kuharibiwa kwa ndege 36 zisizo na rubani za Urusi wakati wa usiku.

"Adui bila shaka alikuwa akilenga miundombinu muhimu na maeneo ya kijeshi kusini mwa nchi," rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema katika Telegram.
"Adui bila shaka alikuwa akilenga miundombinu muhimu na maeneo ya kijeshi kusini mwa nchi," rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema katika Telegram. via REUTERS - SAUDI TV
Matangazo ya kibiashara

Moscow "inaendelea kutishia Ukraine" na imerusha ndege 36 zisizokuwa na rubani, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kwenye Telegram. "Hakuna hata mmoja ya ndege hizi iliyefikia lengo lake," aameongeza, akikaribisha mfumo wa ulinzi wa anga wa nch.

Jeshi la Wanahewa la Ukraine limesema ndege zisizo na rubani aina ya Shahed 136/131 zilizotengenezwa na Iran na Shahed 131 zilirushwa kutoka kaskazini na kusini.

"Adui bila shaka alikuwa akilenga miundombinu muhimu na maeneo ya kijeshi kusini mwa nchi," rais wa Ukraine amesema katika Telegram.

Tangu mapema mwezi Mei, Urusi imezidisha mashambulizi yake ya usiku ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya Ukraine.

Hasa, ilitumia mara mbili makombora ya hypersonic ya Kinjal, ambayo ni ngumu zaidi kuzuia. Kyiv imesema imedondosha ndege 36 kwa kutumia mfumo wa ulinzi wa anga wa Marekani wa Patriot, wa kwanza tangu uvamizi wa Urusi uanze mwezi Februari 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.