Pata taarifa kuu

Ukraine: Vita vya mawasiliano juu ya udhibiti wa Bakhmut

Usiku wa Mei 20 kuamkia 21, Wizara ya Ulinzi ya Urusi na Vladimir Putin mwenyewe walidai kwamba vikosi vya Urusi, vinavyohusishwa na kundi la wanamgambo la Wagner, vinashikilia udhibiti kamili wa mji wa Bakhmut huko Donbass. 

Picha kutoka kwa video iliyochapishwa na idara ya vyombo vya habari vya Prigozhin Jumamosi, Mei 20, 2023, wanachama wa Wagner wakipeperusha bendera ya taifa la Urusi na bendera ya Wagner kwenye jengo lililoharibika huko Bakhmout, Ukraine.
Picha kutoka kwa video iliyochapishwa na idara ya vyombo vya habari vya Prigozhin Jumamosi, Mei 20, 2023, wanachama wa Wagner wakipeperusha bendera ya taifa la Urusi na bendera ya Wagner kwenye jengo lililoharibika huko Bakhmout, Ukraine. AP
Matangazo ya kibiashara

Jumamosi jioni, Wizara ya Ulinzi ilisema kwamba mapigano bado yanaendelea, katika wilaya za mwisho za magharibi mwa jiji. Leo Jumapili asubuhi msemaji wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekanusha kwamba rais huyo alithibitisha kutekwa kwa mji huo. Lakini matokeo ya vita vya Bakhmout pengine yako karibu au yanaweza kuthibitisha hali ya mambo katika uwanja wa vita.

Katika siku za hivi karibuni, jeshi la Ukraine lilidhibiti tu vitalu vya majengo magharibi mwa Bakhmut, labda 5% ya eneo la wilaya, lakini vikosi vya Urusi vimeongeza kasi ya operesheni katika saa 48 zilizopita, hadi kufikia usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, askari wa Ukraine walirekodi video kwenye simu zao, wakitangaza kuanguka kwa jiji hilo, anasema mwandishi wetu wa Kiev, Stéphane Siohan.

Jumamosi jioni, hali ili kuwa tete. Yevgeny Prigozhin, kiongozi wa wanamgambo wa Wagner, alitangaza kutekwa kamili kwa jiji hilo, katika video iliyorekodiwa katikati mwa jiji, akionyesha bendera ya Urusi na bendera ya Wagner.

Suala la wakati

Kwa upande wake, Hanna Malyar, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, anasema kwamba mapigano bado yanaendelea kwenye viunga vya Bakhmut na mamlaka ya Ukraine inakataa kurasimisha kuwa imepoteza mji huo. Leo Jumapili Ukraine pia imebainisha kwamba "imeuzingira kwa kiasi kikubwa" mji huo kutokana na mafanikio ya hivi karibuni ya vikosi vya Kyiv kwenye ukingo wa kaskazini na kusini mwa mji huo. "Kusonga mbele kwa wanajeshi wetu katika vitongoji vya pembezoni, opereshei ambayo inaendelea, kunafanya uwepo wa adui huko Bakhmut kuwa mgumu zaidi. Wanajeshi wetu wameuzingira mji kwa kiasi,” Naibu Waziri wa Ulinzi Ganna Maliar amesema kwenye Telegram.

Kwa kweli, Warusi wanaweza kuwa wamechukua eneo lote la wilaya ya Bakhmout, au wanaweza kuwa karibu ya kulidhibiti, lakini pande hizo mbili zinahusika katika vita vya mawasiliano, wakati wanajeshi wa Ukraine wanafanya wanajibu mashambulizi kaskazini na kusini mwa mwa mji  wa Bakhmut. Kuanguka kwa Bakhmut labda ni suala la saa tu, hali ambayo ni vigumu sema,lakini hii hailezwi ikiwa wanajeshi wa Ukraine wamechukuwa uamuzi wa kujiondoa katika mji huu kwa kuwaangamiza wanajeshi wa Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.