Pata taarifa kuu
VITA-ULINZI

Ukraine: Prigozhin atangaza kukamatwa kamili kwa Bakhmout, jeshi la Ukraine lakanusha

Mkuu wa kundi la wanamgambo wa Urusi Wagner, Yevgeny Prigozhin, amedai Jumamosi Mei 20 kutekwa kamili na watu wake kwa mji wa Bakhmout, kitovu cha mapigano mashariki mwa Ukraine ambayo yamekuwa yakiendelea tangu msimu wa joto uliopita. Jiji "limechukuliwa kwa ukamilifu", amehakikishia katika matangazo ya video kwenye Telegram. Ukraine, bado inadai kudhibiti maeneo ya jiji lakini inabaini kuwepo na hali 'tete'.

Kiongozi wa kundi la wanamgambo la Wagner anatangaza, katika video, kwamba wapiganaji wake wameliteka jiji la Ukraine la Bakhmout, mnamo Mei 20, 2023.
Kiongozi wa kundi la wanamgambo la Wagner anatangaza, katika video, kwamba wapiganaji wake wameliteka jiji la Ukraine la Bakhmout, mnamo Mei 20, 2023. via REUTERS - PRESS SERVICE OF "CONCORD\
Matangazo ya kibiashara

"Mnamo Mei 20, 2023, leo, saa sita mchana, Bakhmout imechukuliwa kwa ukamilifu kutoka mikononoi mwa jeshi la Ukraine": ni kwa maneno haya Yevgeny Prigozhin alitangaza kutekwa kwa jiji hilo katika matangazo ya video na huduma yake ya waandishi wa habari kwenye Telegram. Katika video, kiongozi wa kundi la wanamgambo la Wagner anaonekana pamoja na watu wenye silaha, mbele ya majengo yaliyoharibiwa.

Katika mzozo na uongozi wa kijeshi wa Kremlin, ambao amekosoa mara kadhaa katika wiki za hivi karibuni, Yevgeny Prigozhin anaongeza kuwa "operesheni ya kuudhibiti mji wa Bakhmout imedumu siku 224" na kwamba "wapiganaji wa Wagner ndio wameshiriki pekee".

Ukraine yakanusha na kuzungumzia 'hali mbaya'

Lakini tangazo la Yevgeny Prigozhin lilifuatiwa na tangazo la vikosi vya Ukraine likikanusha madai ya kukamatwa kwa mji wa Bakhmout. "Hali ni mbaya. Wakati huo huo (...) wanaheshi wetu wanadhibiti vifaa na baadhi ya miundombinu ya viwanda katika eneo hilo na vile vile katika sekta ya kibinafsi,” Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Ganna Maliar amesema kwenye Telegram.

Mapigano ya Bakhmout, mji ulioharibiwa katika Oblast ya Donetsk ambayo umuhimu wake wa kimkakati unazozaniwa, ni ndefu na mabaya zaidi ya mzozo ulioanza Februari 2022. Wanajeshi wa Ukraine na Urusi walipata hasara kubwa katika mji huo, wakati mapigano makubwa yanapamba moto katika eneo hilo kwa miezi kadhaa sasa.

Wiki hii Kiev ilidai kuwa imechukua tena zaidi ya kilomita za mraba ishirini kutoka kwa vikosi vya Urusi kaskazini na kusini mwa mji huo, huku ikikiri kuwa wapiganaji wa Wagner wanaendelea kujizatiti vizuri ndani ya jiji lenyewe, ambapo kunaripotiwa kundi dogo tu a upinzani kuelekea magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.