Pata taarifa kuu

Makombora ya Urusi usiku wa kuamkia leo nchini Ukraine yasababisha uharibifu

NAIROBI – Urusi imerusha makombora kadhaa jijini Kyiv na miji mingine ya Ukraine hivi leo na kusababisha majereha na uharibifu mkubwa, kuelekea sikukuu ya kukumbuka ushindi dhidi ya wanajeshi wa Kinazi kutoka Ujerumani.

Urusi imerusha makombora kadhaa jijini Kyiv na miji mingine ya Ukraine hivi leo Jumatatu na kusababisha majereha na uharibifu mkubwa
Urusi imerusha makombora kadhaa jijini Kyiv na miji mingine ya Ukraine hivi leo Jumatatu na kusababisha majereha na uharibifu mkubwa REUTERS - GLEB GARANICH
Matangazo ya kibiashara

Watu watano wamejeruhiwa jijini Kyiv kufutia mashambulio hayo ya jeshi la Urusi, huku moto mkubwa ukiteketeza ghala kubwa la kuhifadhi chakula katika bandari ya Odesa.

Mashambulio haya yanakuja, siku moja kuelekea gwaride kubwa la kijeshi la kila mwaka, litakaloongozwa na rais Vladimir Putin kukumbuka ushindi wake dhidi ya wanajeshi wa Kinazi miaka 70 iliyopita,wakati wa vita vya pili vya dunia.

Jeshi la Ukraine linasema, limefanikiwa kuangusha na kuharibu ndege zisisokuwa na rubani 35 zilizotengezwa nchini Iran ambazo Urusi imekuwa ikirusha usiku kucha katika miji ya Ukraine.

Bandari ya Odesa
Bandari ya Odesa © via REUTERS - OPERATIONAL COMMAND SOUTH PRESS

Jeshi la Urusi pia limerusha makombora yake katika mji wa Bakhtmut, eneo ambalo kwa miezi kadhaa mapigano makali yamekuwa yakishuhudiwa.

Hatua hii ya Urusi inakuja baada ya wiki jana, Kremlin kuituhumu Kyiv kwa kutekeleza jaribio la kumuua rais Putin kwa kutumia ndege zisizo na rubani kwa kushirikiana na Marekani, madai ambayo Washington na Kyvi zilipinga.

Mapigano makali kati ya mamluki wa Wagner na wanajeshi wa Ukraine yamekuwa yakiendelea kwa muda sasa katika mji wa Bakhmut, Donetsk, Ukraine.
Mapigano makali kati ya mamluki wa Wagner na wanajeshi wa Ukraine yamekuwa yakiendelea kwa muda sasa katika mji wa Bakhmut, Donetsk, Ukraine. AP - Roman Chop

Ukraine kwa upande wake ilisema kuwa haina nia ya kushambulia rais Putin bali inapigana kulinda nchi yake na raia wake.

Licha ya hayo, Ukraine imekuwa ikitoa wito kwa nchi washirika wake kuipa silaha zaidi kujilinda kutokana na mashambulio ya Urusi nchini mwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.