Pata taarifa kuu

Viongozi wa Afrika kuwashawishi rais Putin na Zelensky kumaliza vita

NAIROBI – Ujumbe wa viongozi wa bara Afrika wanaojaribu kuzishawishi nchi za Urusi na Ukraine kumaliza mapigano yanayoendelea unatarajiwa kuzuru Moscow na Kiev kuanzia mwezi ujao.

Viongozi wa Afrika kujaribu kutafuta muafaka kati ya Urusi na Ukraine
Viongozi wa Afrika kujaribu kutafuta muafaka kati ya Urusi na Ukraine © DR
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imethibitishwa na ofisa wa ngazi ya juu katika  serikali ya Afrika Kusini, nchi ambayo imeonekana kuwa mshirika wa karibu wa rais Putin.

Wakuu wa nchi za Zambia, Senegal, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Misri na Afrika Kusini, wanatarajiwa kuongoza juhudi hizo, suala ambalo limekaribishwa na umoja wa mataifa.

Katika taarifa yake kwa wabunge, Zane Dangor, katibu katika wizara ya mambo ya nje nchini Afrika Kusini,  tarehe kamili ya ziara hiyo haijatolewa.

Taarifa Zaidi inaeleza kuwa washika dau wengine wanaojaribu kupata suluhu ya mzozo huo ikwemo Marekani tayari wamefahamishwa ambapo wameunga mkono mchakato ulioanzishwa na viongozi hao.

Afrika Kusini ambayo imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na Kremlin, imekataa kuungana na baadhi ya mataifa mengine ya dunia kulaani uvamizi na Urusi nchini Ukraine kwa madai kuwa haigemei upande wowote.

Taarifa hii ya viongozi wa bara Afrika imekuja ikiwa imepita siku chache baada ya kamanda wa jeshi la nchi kavu wa Afrika kusini kufanya ziara nchini Urusi kujadiliana na mwenzake wa Moscow kuhusu ushirikiano wa kijeshi.

Haya yanajiri pia ikiwa imepita siku chache tangu mjumbe wa Marekani mjini Pretoria kuituhumu Afrika kusini kwa kuihami Urusi na silaha za kijeshi mwezi Desemba mwaka jana .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.