Pata taarifa kuu

Ukraine inasema vikosi vya Urusi vimelipua bwawa la Nova Kakhovka huko Kherson

NAIROBI –  Jeshi la Ukraine limesema vikosi vya Urusi vimelipua bwawa kubwa kusini mwa Ukraine, huku afisa anaeegemea upande wa Moscow katika mji wa Nova Kakhovka katika eneo linalodhibitiwa na Urusi katika eneo la Kherson akikanusha madai hayo.

Ukraine inaituhumu Urusi kwa kutekeleza shambulio katika bwawa Kakhovka
Ukraine inaituhumu Urusi kwa kutekeleza shambulio katika bwawa Kakhovka © Maxar Technologies/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Shirika la habari la serikali ya Urusi TASS lilinukuu chanzo kisichojulikana kilicho karibu na suala hilo kikisema kuwa bwawa hilo liliharibiwa na eneo hilo lilikuwa na mafuriko.

Shirika lengine habari la serikali ya Urusi, RIA Novosti, lilimnukuu meya wa Nova Kakhovka aliyewekwa rasmi na Moscow akisema bwawa hilo liliharibiwa na makombora aliyoilaumu Ukraine.

Utawala wa kijeshi wa Ukraine katika eneo la Kherson ulitoa wito kwa watu kuwa tayari kuhama kutoka vijiji kadhaa kwenye ukingo wa kulia wa Mto Dnieper huku kiwango cha maji kikiongezeka kufuatia uharibifu wa bwawa hilo.

Rais Volodymyr Zelensky amewatuhumu wanajeshi wa Urusi kwa kutekeleza uharibifu wa bwawa hilo analosema limeharibiwa na magaidi wa Moscow.

Ukraine inasema jeshi lake linapiga hatua na kusonga mbele, kwa lengo la kuudhibiti mji wa Bakhmut, ambao kwa miezi kadhaa sasa, kumekuwa na mapigano makali na vikosi vya Urusi.

Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Hanna Maliar amethibitisha kusonga mbele kwa vikosi vya nchi yake, lakini hajasema iwapo operesheni maalum inalenga kudhibiti maeneo yake yanayoshikiliwa na wanajeshi wa Urusi, imeanza.

Rais Volodymyr Zelensky kupitia ujumbe wake wa Video, amewashukuru wanajeshi wa nchi yake kwa kile alichokisema, wameanza kurejesha matumaini, akisisitiwa kuwa anadui kwa maana ya Urusi, anajua kuwa Ukraine itashinda.

Katika hatua nyingine, Urusi nayo inasema siku jana ilifanikiwa kuzuia shambulio jipya kutoka kwa wanajeshi wa Ukraine katika jimbo la Donetsk, lakini taarifa hii haijathibitishwa kama ni sahihi.

Siku chache zilizopita, Ukraine ilitangaza kuwa sasa iko tayari kuanza mapambano makali dhidi ya wanajeshi wa Urusi ili kuchukua maeneo yote ya Mashariki likiwemo jimbo la Donetsk lililochukuliwa baada ya nchi yao kuvamiwa mwaka uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.