Pata taarifa kuu

Italia: Wanne wafariki akiwemo Muisraeli katika ajali ya boti kwenye Ziwa Maggiore

Watu wanne, ikiwa ni pamoja na Muisraeli, wamekufa maji katika tukio ajali ya boti ya watalii iliyozama kwenye Ziwa Maggiore kaskazini mwa Italia, ajali ambayo imesababishwa na upepo mkali, kulingana na kikosi cha Zima moto.

Ziwa Maggiore, ambalo liko kusini mwa Alps, ni ziwa la pili kwa ukubwa nchini Italia na kivutio maarufu cha watalii.
Ziwa Maggiore, ambalo liko kusini mwa Alps, ni ziwa la pili kwa ukubwa nchini Italia na kivutio maarufu cha watalii. Getty Images / Mats Silvan
Matangazo ya kibiashara

Boti hiyo yenye urefu wa mita 16 ilikuwa ikisafiri kwenye pwani ya Lisanza, kusini mwa ziwa Jumapili jioni wakati hali ya hewa ilipozidi kuwa mbaya, huku dhoruba kali ikipiga.

"Miili ya watu wanne imepatikana," msemaji wa kikosi cha Zima moto Luca Cari ameliambia shirika la habari la AFP.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel, mmoja wa waliofariki ni raia wa Israel mwenye umri wa miaka 'hamsini'.

Kulingana na tovuti ya habari ya mtandaoni ya Varese News, wahanga wengine ni raia wa Urusi na Waitaliano wawili.

Rais wa jimbo la Lombardy, Attilio Fontana, aliema anasikitishwa na 'tukio mbaya' lililosababishwa na 'kimbunga'.

Takriban abiria 20 walionusurika walitolewa majini na boti nyingine na wengine waliweza kuogelea hadi ufukweni, vyombo vya habari vya Italia vimeripoti.

Boti hiyo ilikuwa imebeba watalii wa Kiitaliano na wa kigeni na ilizama haraka, akiwemo mmoja wa wahanga, kulingana na habari za vyombo vya habari.

Ziwa Maggiore, ambalo liko kusini mwa milima, ni ziwa la pili kwa ukubwa nchini Italia na kivutio maarufu cha watalii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.