Pata taarifa kuu

Italia: Zaidi ya watu 36,000 watoroka makazi yao kutokana na mafuriko

Zaidi ya watu 36,000 wamelazimika kuyahama makazi yao kufuatia mafuriko yaliyoharibu maeneo ya kaskazini-mashariki mwa Italia, manipa ya mji wa Emilia-Romagna imelitangaza siku ya Jumamosi, huku mafuriko yakikumba nyumba nyingi na vitongoji vikikumbwa na maporomoko mapya ya ardhi.

Mafuriko hayo yalisababisha maporomoko ya udongo zaidi ya 305 na kuharibu au kukata zaidi ya barabara 500 mkoani humo.
Mafuriko hayo yalisababisha maporomoko ya udongo zaidi ya 305 na kuharibu au kukata zaidi ya barabara 500 mkoani humo. AP - Luca Bruno
Matangazo ya kibiashara

Hali mbaya ya hewa iliyoathiri eneo la Emilia-Romagna imeua watu kumi na wanne na kubadilisha mitaa ya miji kuwa mito.

Mamlaka ya mkoa imeongeza hadi Jumapili tahadhari ya hali ya hewa nyekundu.

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni ametangaza siku ya Jumamosi kwamba ataondoka kwenye mkutano wa kilele wa G7 huko Hiroshima, Japan na kurejea Italia ili kushughulikia mzozo huo.

"Kusema ukweli, siwezi kukaa mbali sana na Italia katika wakati mgumu kama huu," ameuambia mkutano wa waandishi wa habari, akiwashukuru watu 5,000 - wanachama wa timu za uokoaji na watu wa kujitolea - ambao wanasaidia waathiriwa waliokumbwa na mafuriko.

Pia amewashukuru wenzake wa G7 kwa kutoa msaada.

Bi Meloni anatarajiwa kuzuru maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko siku ya Jumapili.

Mamlaka ya Ravenna Jumamosi imeamuru watu kuhamishwa mara moja kutoka vitongoji vilivyokumbwa na mafuriko.

Helikopta iliyokuwa ikishiriki katika majaribio ya kurejesha umeme ilianguka karibu na eneo la Lugo siku ya Jumamosi, na kumjeruhi mmoja wa watu wanne waliokuwa ndani, ya helikopta hiyo, kikosi cha Zima Moto kimesema.

Mafuriko hayo yalisababisha maporomoko ya udongo zaidi ya 305 na kuharibu au kukata zaidi ya barabara 500 mkoani humo.

"Maji yalianza kupanda saa 2:00 usiku (Ijumaa) yakivuka mashamba", baada ya mifereji ya maji iliyo karibu kufurika, na kuzamishwa na maji ya mito iliyofurika, Mauro Lodola, fundi umeme toka miaka 54, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.