Mafuriko nchini Italia yaua watu 14, 'bustani' ya nchi hiyo ikiwa imeharibiwa
Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko imeongezeka hadi 14 huko Emilia-Romagna, eneo tajiri linalochukuliwa kuwa "bustani ya matunda ya Italia". Uharibifu wa nyenzo na kilimo pia ni wa kiwango cha nadra, ishara, kulingana na mamlaka, ya mabadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea.
Imechapishwa:
Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yanayoikumba Emilia-Romagna imeongezeka. Takriban watu 14 wamefariki katika eneo hili tajiri la kilimo na kitalii kaskazini mwa Italia, viongozi wa eneo hilo wamesema Ijumaa Mei 19.
Waokoaji bado walikuwa wakifanya kazi ya kuwahamisha watu waliokwama katika nyumba zao zilizozingirwa na mafuriko na mvua ilianza kunyesha tena baada ya zaidi ya saa 24 za utulivu.
Huko Ravenna, viongozi wameagiza "kuondoka haraka" katika maeneo kadhaa Ijumaa asubuhi na kutoa wito kwa raia "kuhama tu ikiwa ni lazima".
(Pamoja na AFP)