Pata taarifa kuu

Italia: Saba wafariki kutokana na hali mbaya ya hewa

Takriban watu saba wamefariki kutokana na hali mbaya ya hewa iliyopiga katikati mwa Italia usiku wa Alhamisi Septemba 15 kujaa maji, mamlaka ya ulinzi wa raia imesema. "Kulingana na manispaa ya jiji hilo, tuna idadi ya awali ya watu waliofariki dunia. Mwili wa saba umepatikana hivi punde,” msemaji wa Fabrizio Curcio, mkuu wa mamlaka ya ulinzi wa raia nchini Italia, ameliambia shirika la habari la AFP, akithibitisha taarifa kutoka kwa vyombo vya habari vya Italia.

Wakazi wa eneo hilo wakifanya usafi baada ya mafuriko huko Castelletto D'Orba nchini Italia, Oktoba 22, 2019.
Wakazi wa eneo hilo wakifanya usafi baada ya mafuriko huko Castelletto D'Orba nchini Italia, Oktoba 22, 2019. Équipe locale / REUTERS TV
Matangazo ya kibiashara

Mafuriko makubwa yamekumba eneo la Marche katikati mwa Italia. Kulingana na mamlaka ya ulinzi wa raia milimita 420 za mvua zimenyesha kwa saa kadhaa.

Watu wengine watatu pia hawajulikani waliko, akiwemo mtoto wa miaka sita ambaye alikuwa na mama yake kwenye gari. Mwaname huyo aliokolewa na maafisa wa idara ya Zima Moto lakini nguvu ya mkondo wa maji ilimchukua mtoto wake, kulingana na mamlaka ya ulinzi wa raia. Eneo lililoathiriwa zaidi ni jimbo la Ancona, bandari ilioko kwenye Bahari ya Adriatic, lakini hali mbaya ya hewa pia imekumba eneo jirani la Umbria.

Katika jimbo la Ancona, maeneo mengi yamekosa umeme na shule zitafungwa leo Ijumaa katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi. Kulingana na Corriere della Sera, takriban milimita 400 za mvua zilinyesha Alhamisi jioni katika muda wa saa mbili, kiasi ambacho kwa kawaida hunyesha katika muda wa miezi sita katika eneo hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.