Pata taarifa kuu

Mvutano wa kidiplomasia waibuka kati ya Poland na Urusi

NAIROBI – Taifa la Poland Jumamosi, Aprili 29, limesema kuwa limeteka jengo la shule ya upili karibu na ubalozi wa Moscow huko Warsaw, kwa ajili ya watoto wa wanadiplomasia, hatua ambayo Urusi imeitamka kuwa kinyume cha sheria.

Polisi wa Poland, nje ya shule ya upili ya zamani ya Urusi huko Warsaw, Poland, Aprili 29, 2023.
Polisi wa Poland, nje ya shule ya upili ya zamani ya Urusi huko Warsaw, Poland, Aprili 29, 2023. AFP - JAAP ARRIENS
Matangazo ya kibiashara

Mzozo juu ya jengo la ghorofa nyingi la miaka ya 1970, lililopewa jina la kiota cha kijasusi na raia wa Warsaw, umekuwa ukiendelea kwa mwaka mmoja.

Jengo hili ni la jumba la jiji la Warsaw, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Poland, Lukasz Jasina ameiambia AFP, akiongeza kuwa hatua hiyo ilifuata agizi kuu.

Poland inasema kuna tofauti kubwa katika idadi ya majengo ya kidiplomasia ambayo kila mmoja alikuwa nayo katika nchi nyingine.

Kwa upande wake, Urusi imesema uvamizi huu wa Poland ni ukiukaji wa wazi wa makubaliano ya kimataifa na kuonya kuhusu athari kubwa zitakazotokana na uvamizi huu.

Tunachukulia hili kama kitendo kingine cha chuki kutoka kwa mamlaka ya Poland na ukiukaji wa wazi wa mkataba wa Vienna wa 1961, wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema.

Wizara hiyo imeongeza kuwa uvamizi huu hautabaki bila majibu makali ya Urusi, na vilevile itakuwa na athari kwa mamlaka ya Poland na maslahi ya Poland nchini Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.