Pata taarifa kuu

Urusi yatishia kusitisha mpango wa mauzo ya nafaka kutoka Ukraine

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov yuko Uturuki Ijumaa hii, Aprili 7, mwanachama wa NATO ambaye anasimama wazi kwa uhusiano wake mzuri na Moscow na jukumu lake kama mpatanishi katika vita vya Ukraine. 

Mjini Ankara, Uturuki, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov ametishia kusitisha makubaliano tete ya mpango wa mauzo ya nafaka kutoka Ukraine mnamo Ijumaa, Aprili 7.
Mjini Ankara, Uturuki, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov ametishia kusitisha makubaliano tete ya mpango wa mauzo ya nafaka kutoka Ukraine mnamo Ijumaa, Aprili 7. REUTERS - CAGLA GURDOGAN
Matangazo ya kibiashara

Sergei Lavrov amekutana na mwenzake wa Uturuki, Mevlüt Cavusoglu. Wote wamejadili masuala mengi ya nchi mbili na kikanda. Lakini vita vya Ukraine na mpango wa nafaka kutoka Ukraine ndivyo mawaziri wamejadili kwa kina a kutoa maoni yao mengi tu.

Na mwanahabari wetu mjini Istanbul, Anne Andlauer

Mnamo Machi 18, baada ya mazungumzo makali, Urusi ilikubali kurefusha kwa siku sitini makubaliano ya Julai 2022 ya kuiruhusu Ukraine kuuza nje nafaka zake kupitia Bahari Nyeusi. Siku 60 badala ya 120, kama ilivyotarajiwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, mfadhili wa makubaliano hayo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Urusi inalalamika juu ya matengenezo ya vikwazo kwa mauzo yake ya bidhaa za kilimo na mbolea. Ingawa bidhaa hizi haziko chini ya vikwazo vya nchi za Magharibi, vikwazo vinapunguza ufikiaji wa wasafirishaji wa Urusi kwa ufadhili, bima na bandari. Kutoka Ankara, Sergei Lavrov ametishia bila moja kwa moja kutofanya upya makubaliano hayo baada ya siku 60 kumalizika:

"Ikiwa hawana nia ya kutekeleza kwa uaminifu kile Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekuwa akipendekeza na kuendeleza, waache waendelee kusafirisha bidhaa kutoka Ukraine kwa nchi kavu, kwa nji ya reli na baharini. Tayari wameweka vifaa. Ikibidi, tutafanya kazi nje ya wigo wa mpango huu. Tuna uwezo wa kufanya hivyo na Uturuki na Qatar. Marais wameshajadili mipango hii. Usafirishaji wetu kwa nchi zinazohitaji hautaathiriwa. Ninaahidi. "

Kando yake, mwenzake wa Uturuki Mevlüt Cavusoglu aliunga mkono matakwa ya Urusi: “Marekani na Uingereza zimechukua baadhi ya hatua kuhusu suala la ufadhili na bima, lakini tatizo linaendelea. Vile vile, baadhi ya hatua zimechukuliwa kusafirisha mbolea ya Urusi kwa nchi za Afrika kupitia baadhi ya nchi za Magharibi kama vile Uholanzi, Estonia au Latvia, lakini si kila kitu kimetatuliwa. Tunapaswa kusema, tunapaswa kuwa waadilifu. Tunaposema hivyo, wengine wanatuuliza ikiwa tunaunga mkono Urusi. Hapana. Muhimu ni kuendelea kwa makubaliano haya. "

Tangu kuanza kutekelezwa, makubaliano hayo yameruhusu kuuzwa nje ya nchi kwa zaidi ya tani milioni 27 za mahindi, ngano na nafaka nyinginezo kwenye masoko ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.