Pata taarifa kuu

Makubaliano kuhusu nafaka kutoka Ukraine yarefushwa hadi majira ya baridi

Makubaliano ya nafaka yaliyotiwa saini mnamo mwezi Julai kati ya Kyiv na Moscow kuruhusu kuendelea kwa mauzo ya nafaka ya Ukraine kupitia Bahari Nyeusi yataongezwa muda wa siku 120 kuanzia tarehe 19 Novemba 2022. Hii ilmetangazwa Alhamisi na Waziri wa Miundombinu wa Ukraine, akikaribisha "hatua muhimu katika mapambano dhidi ya mzozo wa chakula duniani".

Makubaliano ya kuwezeshavmauzo ya nafaka ya ukraine kutoka bandari ya Ukraine yamerefushwa kwa miezi minne ya majira ya baridi.
Makubaliano ya kuwezeshavmauzo ya nafaka ya ukraine kutoka bandari ya Ukraine yamerefushwa kwa miezi minne ya majira ya baridi. Danil SEMYONOV / AFP
Matangazo ya kibiashara

Habari za kurefushwa kwa makubaliano hayo zimethibitishwa mara moja na Uturuki, mpatanishi mkuu wa makubaliano hayo. Makubaliano haya yanahitimishwa chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa na utekelezaji wake sahihi unahakikishwa kutoka kwa kituo cha uratibu kilichoko Istanbul, anaripoti mwandishi wetu huko Istanbul, Anne Andlauer.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres 'amekaribisha' habari hiyo katika taarifa kutoka kwa Kituo cha Uratibu wa Pamoja chenye makao yake makuu mjini Istanbul (JCC), ambacho kinasimamia harakati za meli kupitia Bosphorus.

Wakati Ukraine na Urusi kila moja ilitia saini makubaliano haya ya nafaka mnamo Julai 22 huko Istanbul, nakala inatoa upanuzi wake wa moja kwa moja baada ya siku 120, isipokuwa mmoja wa wahusika ataamua. Muda wa mkataba huo haujulikani, hata hivyo, wakati Urusi ilisitisha ushiriki wake kwa siku chache kati ya mwishoni mwa mwezi Oktoba na mapema mwezi Novemba. Ulirejea katika mkataba huobaada ya shughuli kali za kidiplomasia kati ya Moscow na Ankara.

Tani milioni 11 za mazao ya kilimo nje ya nchi katika muda wa miezi minne

Siku ya Jumatano, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alionekana kuwa na matumaini, akitumai kurefushwa kwa makubaliano hayo kwa mwaka mmoja. Hii ndio Ukraine ilitaka. Hatimaye itakuwa siku 120, chini ya hali sawa. Umoja wa Mataifa, ambao pia ni sehemu ya makubaliano hayo, ulijitangaza "kujitolea kikamilifu kuondoa vikwazo vinavyozuia usafirishaji wa bidhaa za kilimo na mbolea za Urusi", hatua ambayo Recep Tayyip Erdogan pia alisema alikuwa makini sana.

Katika muda wa chini ya miezi minne, makubaliano yaliwezesha mauzo ya nje ya zaidi ya tani milioni 11 za bidhaa za kilimo za kutoka Ukraine. Kabla ya kuondoka au kuingia katika Bahari Nyeusi, meli zote hukaguliwa nje ya Istanbul na timu inayoundwa na Warusi, Waukraine, Waturuki na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa.

Nafaka hizi ni muhimu kwa kuleta utulivu wa bei katika masoko ya kimataifa na kuwapa watu walio hatarini zaidi na hatari ya njaa, hasa barani Afrika. Kati ya tani milioni 11 zilizosafirishwa hadi sasa, karibu 40% zimeenda kwa nchi zinazoendelea.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.