Pata taarifa kuu

IMF yaidhinisha mpango wa msaada wa dola bilioni 15 kwa Ukraine

Mpango huu wa msaada uliotiwa saini wiki mbili zilizopita na serikali ya Ukraine ni sehemu ya bahasha kubwa ya dola bilioni 115. Kuthibitishwa kwa msaada huu mpya kunaruhusu kutolewa kwa awamu ya kwanza ya dola bilioni 2.7.

Nembo ya Shirika la Fedha la Kimataifa.
Nembo ya Shirika la Fedha la Kimataifa. AP - Andrew Harnik
Matangazo ya kibiashara

Lengo la usaidizi huu mpya wa dola milioni 15.6 mwanzoni ni kuwezesha Ukraine kuunganisha bajeti yake ya mwaka 2023, lakini pia kuimarisha rasilimali zake za kifedha na kupunguza mfumuko wa bei.

Kuhusu msaada wa jumla kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) la dola bilioni 115 katika kipindi cha miaka minne, lina vipengele kadhaa: bilioni 2 katika kufutwa kwa sehemu ya deni lililopo, msamaha wa madeni wa bilioni 20, mikopo ya bilioni 60 na misaada ya bilioni 20, kulingana na IMF.

Ujenzi upya

Kwa fedha hizi, Ukraine inapaswa kuhakikisha kuanza maisha mapya baada ya vita na ujenzi mpya. IMF inatarajia kufufua uchumi taratibu mwaka huu nchini Ukraine. Lakini pia inaona hali mbaya zaidi, ikiwa vita vitaendelea hadi mwisho wa mwaka 2025.

Ukraine imeungwa mkono na taasisi za kifedha tangu kuanza kwa mashambulizi ya Urusi Februari 24, 2022. Benki ya Dunia ililipa dola bilioni 20, Marekani dola bilioni 110, kwa msaada wa kijeshi. Hii imeruhusu nchi kuweka huduma zake za umma sawa au kulipa mishahara ya watumishi wa umma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.