Pata taarifa kuu

Vladimir Putin: Vikwazo 'huenda' vikawa na matokeo 'hasi' kwa uchumi wa Urusi

Rais wa Urusi Vladimir Putin amekiri Jumatano kwamba vikwazo vya kimataifa vinavyolenga Moscow kwa mashambulizi yake nchini Ukraine "huenda" vikawa na matokeo "hasi" katika "muda wa kati" kwa uchumi wa taifa, baada ya kusifu katika miezi ya hivi karibuni marekebisho ya Urusi dhidi ya vikwaz hivyo.

Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano na kiongozi wa sehemu ya chama cha United Russia na mjumbe wa kamati ya usalama ya Baraza la Bunge (Duma) Vladimir Vasiliev huko Kremlin huko Moscow, Urusi Machi 22, 2023.
Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano na kiongozi wa sehemu ya chama cha United Russia na mjumbe wa kamati ya usalama ya Baraza la Bunge (Duma) Vladimir Vasiliev huko Kremlin huko Moscow, Urusi Machi 22, 2023. via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

"Vikwazo vilivyowekwa kwa uchumi wa Urusi katika muda wa kati vinaweza kuwa na athari mbaya kwake," ameonya rais wa Urusi wakati wa mkutano na serikali uliorushwa kwenye televisheni.

Hayo yanajiri wakati Jana Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema wanajeshi wa Urusi wanakishikilia mateka kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia na kwamba usalama wake hautaweza kuhakikishwa hadi pale watakapoondoka eneo hilo.

Naye Mkuu wa diplomasia ya Ukraine Dmytro Kouleba siku ya Jumanne aliitaka Moscow kujiondoa kutoka "kila mita ya mraba" ya Ukraine, akisisitiza kwamba hakuwezi kuwa na amani na Urusi 'kwa hali yoyote'.

"Nataka kuwa wazi kabisa, Urusi lazima ijitoe katika kila mita ya mraba ya eneo la Ukraine. Hakuwezi kuwa na maelewano kuhusu maana ya neno kujiondoa," alisema Kouleba, ambaye alikuwa akizungumza katika mjadala wa jukwaa la "amani nchini Ukraine" chini ya mwamvuli wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.