Pata taarifa kuu

Mapigano nchini Ukraine yalianzaje

NAIROBI – Ni mwaka mmoja kamili, tangu Urusi ilipoivamia jirani yake Ukraine, katika vita vinavyoelezwa kuwa vikubwa zaidu barani Ulaya, tangu kumalizika kwa vita vya pili ya dunia.

Ni mwaka mmoja sasa tangu Urusi kuivamia Ukraine
Ni mwaka mmoja sasa tangu Urusi kuivamia Ukraine © Felipe Dana / AP
Matangazo ya kibiashara

Miezi kadhaa kabla ya uvamizi huo, Urusi ilianza mazoezi ya kijeshi katika mpaka na Ukraine, huku jitihada za Kimataifa za kidiplomasia, kuzuia uvamizi huo, zikigonga mwamba.

Ilipofika Februari tarehe 24, wanajeshi wa Urusi waliingia Ukraine wakiwa kwenye magari ya kijeshi na kuanza mashambulio, yalizua wasiwasi na kusabisha wakaazi wa maeneo ya Mashariki, kuanza kukimbilia katika mataifa jirani.

Rais Vladmir Putin katika hotuba aliyoitoa kwa taifa na kufuatiliwa kote duniani, alieleza uvamizi huo kama operesheni za kijeshi katika nchi aliyosema ni sehemu ya Urusi, na kuhoji ulali wake kama taifa.

Mwaka mmoja baadaye, maelfu ya watu wameuawa na zaidi ya Milioni nane kukimbia Ukraine kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, na licha ya Mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Urusi, rais Putin amekataa kuachana na uvamizi huo.

Kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja, Ukraine imekuwa ikishinikiza washirika wake, kuipa silaha za kuishinda Urusi, msaada ambao imekuwa ikipata pamoja na ule wa fedha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.