Pata taarifa kuu

Kremlin: 'Vita vya mseto' kati ya Urusi na Wamagharibi vitadumu 'muda mrefu

"Vita vya mseto" kati ya Moscow na mataifa yenye nguvu ya Magharibi kuhusu mzozo wa Ukraine "vitadumu kwa muda mrefu", Kremlin imesema Jumatano, zaidi ya mwaka mmoja baada ya wanajeshi wa Urusi kuanzisha vita dhidi ya nchi hiyo jirani.

Ikulu ya Kremlin inasema 'vita vya mseto' kati ya Moscow na mataifa yenye nguvu ya Magharibi kuhusu mzozo wa Ukraine 'vitadumu kwa muda mrefu'.
Ikulu ya Kremlin inasema 'vita vya mseto' kati ya Moscow na mataifa yenye nguvu ya Magharibi kuhusu mzozo wa Ukraine 'vitadumu kwa muda mrefu'. AP - Alexander Zemlianichenko
Matangazo ya kibiashara

"Ikiwa tunazungumza juu ya vita kwa maana pana, juu ya makabiliano na nchi zisizo za kirafiki, zenye uhasama, kuhusu vita hivi vya mseto (...), basi vitadumu kwa muda mrefu," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari, huku akisisitiza kwamba "Warusi wameshikamana na Rais" Vladimir Putin.

Hayo yanajiri wakati Rais wa Urusi Vladimir Putin amekiri Jumatano kwamba vikwazo vya kimataifa vinavyolenga Moscow kwa mashambulizi yake nchini Ukraine "huenda" vikawa na matokeo "hasi" katika "muda wa kati" kwa uchumi wa taifa, baada ya kusifu katika miezi ya hivi karibuni marekebisho ya Urusi dhidi ya vikwaz hivyo.

"Vikwazo vilivyowekwa kwa uchumi wa Urusi katika muda wa kati vinaweza kuwa na athari mbaya kwake," ameonya rais wa Urusi wakati wa mkutano na serikali uliorushwa kwenye televisheni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.