Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Ufaransa: Vigogo wa walio wengi waungana na Macron kutafuta njia ya kuondokana na mzozo

Katika mkesha wa siku ya kumi ya maandamano dhidi ya mageuzi ya pensheni na baada ya makabiliano makali huko Sainte-Soline siku ya Jumamosi, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anakutana Jumatatu hii mchana na sehemu ya serikali yake na viongozi wa wengi katika ikulu ya Élysée. Rais wa Ufaransa anatafuta njia ya kuondokana na mgogoro huo, huku maandamano yakizidi kushika kasi. Serikali imeshindwa kutuliza hasira ya waandamanaji.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akipigwa picha kwenye Ikulu ya Élysée huko Paris mnamo Machi 24, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akipigwa picha kwenye Ikulu ya Élysée huko Paris mnamo Machi 24, 2023. © AP - Thomas Padilla
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa  anawaita vigogo kutoka kambi yake kwa ajili ya mkutano husiana na mgogoro unaoendelea. Waziri Mkuu Élisabeth Borne, François Bayrou na Édouard Philippe watakuwepo.

Na mawazo yote mazuri yanakaribishwa. Kwa sababu serikali imeshindwa kutuliza hasira za wananchi. Mahojiano ya televisheni na Mkuu wa Nchi siku ya Jumatano hayakupunguza kasi ya uhamasishaji wa wapinzani.

Badala yake, kulikuwa na watu wengi zaidi mitaani Alhamisi ya wuki iliyopita.

Kwa hivyo, kusbiri mwezi mmoja na uamuzi wa Baraza la Katiba juu ya mageuzi, kama ilivyopangwa na rais wa Jamhuri, haiwezekani tena.

Bw. Macron atapitia nakala yake na kutafuta mkakati mpya. Kuanzisha upya mazungumzo haraka na vyama vya wafanyakazi ni muhimu ili kupunguza hali ya wasiwasi nchini.

Kufanya kinachowezekana haraka iwezekanavyo ili kurejesha udhibiti haraka

Kwa upande wake, Bi Borne anasema yuko tayari kupokea miungano hiyo. Waziri Mkuu pia atazindua mashauriano wiki ya Aprili 3 na makundi ya wabunge na vyama vya siasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.