Pata taarifa kuu

Ufaransa: Mageuzi ya pensheni ni 'muhimu', asema Emmanuel Macron

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amenaini Jumatano Machi 22 kwamba mageuzi yake ya pensheni ambayo yanapingwa yanapaswa 'kuanza kutumika mwishoni mwa mwaka' kwa sababu ni ya 'muhimu'. Amesema hayo wakati wa mahojiano ya televisheni kwenye TF1 na France 2, huku raia wenye hasira wakiendelea kupinga mpango wake wa mageuzi yapensheni.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza wakati wa mahojiano ya televisheni katika Ikulu ya Elysee huko Paris mnamo Machi 22, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza wakati wa mahojiano ya televisheni katika Ikulu ya Elysee huko Paris mnamo Machi 22, 2023. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

"Mageuzi haya, ni ya muhimu, hayanifurahishi, ningependa kutoyafanya, lakini pia ndiyo maana nilijitolea kuyafanya", ametangaza Emmanuel Macron, Jumatano hii Machi 22, kwenye televisheni za TF1 na France 2, akitaka mageuzi hayo kuanza kutumika ifikapo mwisho wa mwaka "ili mambo yawe sawa". "Hakuna suluhu 36," amesisitiza.

Rais amesema yuko tayari "kupoteza uaminifu" lakini aweze kutekeleza mageuzi haya: "Mimi, sitaraji kuchaguliwa tena (...), lakini kati ya uchaguzi wa muda mfupi na masilahi ya jumla ya nchi, nachagua maslahi ya jumla ya nchi”, amebaini Bw. Macron, akiongeza kuwa "ikiwa ni muhimu nyuma ya kuidhinisha mageuzi haya kutopendwa leo, nitaidhinisha". Rais Emmanuel Macron amesema anasikitishwa na vyama vya wafanyakazi ambavyo havijawasilisha 'pendekezo la maelewano' juu ya nakala ya mageuzi, akisisitiza kwamba serikali ilifanya, kwa upande mwingine, 'na Bunge'.

'Si upinzani wala makundi'

'Hatuwezi kukubali ama upinzani au makundi' baada ya kupitishwa kwa mageuzi ya pensheni kwa Ibara ya 49.3 ya katiba, ameongeza Emmanuel Macron, akilaani miongoni mwa waandamanaji "makundi yanayotumia vurugu". "Wakati Marekani ilishuhudia ukile wkilichotokea Capitol Hill, wakati Brazili ilishuhudia kile kilichotokea nchini humo (...), nawaambia waziwazi", "hatuwezi kukubali waasi wala makundi", amesema rais Macron kwa kurejelea matukio ya uasi yaliyoshuhudiwa na taasisi hizo katika nchi hizi mbili. "Hatutavumilia maovu yoyote," ameogeza.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.