Pata taarifa kuu

Macron aazimia kuptisha mfumo wa pensheni kwa kutumia kifungu cha katiba

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amechagua kutumia kifungu cha 49.3 cha katiba ya Ufaransa baada ya mikutano kadhaa na viongozi wakuu, akiwemo Waziri Mkuu Elisabeth Borne, baada ya kubaini kwamba hakukuwepo na wabunge wengi wa kupitisha mageuzi hayo.

Waziri Mkuu Élisabeth Borne amejihusisha na jukumu la serikali kutumia kifungu cha 49.3cha katiba ili mageuzi ya pensheni yaidhinishwe.
Waziri Mkuu Élisabeth Borne amejihusisha na jukumu la serikali kutumia kifungu cha 49.3cha katiba ili mageuzi ya pensheni yaidhinishwe. REUTERS - PASCAL ROSSIGNOL
Matangazo ya kibiashara

Vyanzo kadhaa vilivyo karibu na ofisi ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron vimeliambia shirika la habari la AFP kwamba rai huyo atatumia uwezo wa kikatiba unaoiwezesha serikali kuwapiku wabunge.

Jana Alhamisi, polisi walikabiliana na waandamanaji jijini Paris, baada ya serikali ya rais Emmanuel Macron kuamua kupita kwa mageuzi ya mfumo wa pensheni nchini humo bila kupigiwa kura bungeni. 

Miongoni mwa mageuzi hayo, ni kuongeza muda wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64. Vyama vya wafanyakazi, vimeendelea kuandaa maandamano kupinga mageuzi hayo. 

Waziri Mkuu Elizabeth Borne, ameelezea masikitiko yake baada ya kuzomewa na wabunge wa upinzani kwa kutumia kifungo cha katiba kuwazuia wabunge kupiga kura.

Kutokana na hatua hii, mwanasiasa wa upinzani kutoka mrengo wa kulia Marine Le Pen, amependekeza kuwasilishwa kwa mswada wa kukosa imani na rais Macron. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.